Habari za Punde

MAMLAKA YA MAPATO TRA YAHIMIZA UMUHIMU WA KULIPA KODI KWA JUMUIYYAZAANI

Afisa msimamizi wa kodi (TRA)  Abdalla Seif Abdalla akijibu maswali yaliyoulizwa na washiriki wa semina ya utozaji kodi kwa Taasisi za dini na hisani huko Ukumbi wa Sanaa Raha leo . 
Na Kijakazi Abdalla  Maelezo  Zanzibar. 11/03/2020
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamewaomba viongozi wa taasisi za dini na hisani kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na taasisi hiyo katika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa ulipaji kodi nchi.
Hayo ameyasema na Afisa Mwandamizi wa Huduma na Elimu Shuweikha Salum Khalfan huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo wakati akiwasilisha mada ya utozaji kodi kwa taasisi za dini na Hisani .
Amesema kulipa kodi ni alama ya uzalendo na sio adhabu kwani mpango wa kuongeza mapato ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo nchini.
“Kulipa kodi ni alama ya uzalendo na sio adhabu ni mpango wa Serikali kuipeleka mbele nchi kimapato na kukua uchumi wake”, alisema Afisa huyo.
Aidha amesema kulipa kodi ni mchango wa lazima ambao umewekwa kisheria kwa raia na wageni kwa lengo la kukusanya mapato kwa ajili ya matumizi ya Taifa.
Afisa huyo ameeleza kuwa Serikali hukusanya kodi kwa jamii kwa lengo la kutoa huduma mbalimbali za kijamii ili kuleta maendeleo nchini.
Hata hivyo amefahamisha kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imepewa jukumu la kutoa taarifa na takwimu za kulipa kodi na mapao yanayokusanya Zanzibar hupelekwa katika mfuko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (Hazina).
Kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa Kodi Mamlaka hiyo amesema kuna baadhi ya taasisi za hisani hutumia mwavuli wa jumuia za dini kutozisajili taasisi zao jambo ambalo hupelekea kukosa misaada
Aidha amezitaka taasisi za dini na hisani kuzijasili taasisi zao katika Mamlaka ya Mapato TRA kwa lengo la kupata taarifa zao na kuweza kuweza kufaidika na huduma hiyo.
Afisa Mwandamizi wa huduma na elimu (TRA)  Shuwekha Salum Khalfan akiwasilisha mada kuhusu utozaji kodi kwa Taasisi za dini  na hisani katika semina iliofanyika Ukumbi wa Sanaa Raha leo Zanzibar. 
Amiri kutoka Jumuiya ya walimu wa madrasa za qur-an Zanzibar  (WAMAQU) Sheikh Hamad Mbarouk Said akichangia mada juu ya utozaji wa kodi  kwa taasisi za dini na hisani katika Ukumbi wa Sanaa Raha leo Zanzibar. 
Katibu Tawala ANGOZA Nuhu  Machano Ali akichangia mada juu ya utozaji kodi kwa Taasisi za dini  na hisani katika semina iliofanyika ukumbi wa Sanaa Raha leo . 
Picha Na Fauzia Mussa – Maelezo Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.