Habari za Punde

Manispaa Wilaya ya magharibi B kufanya usafi usiku na mchana

Na Takdir Suweid, Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ . 

 Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ Ali Abdallah Natepe amesema wameweka Mikakati ya kufanya Usafi Usiku na Mchana ili kuviongezea nguvu Vikundi vinavyofanya kazi wakati wa Asubuhi. 

 Akizungumza kwa Niaba yake huko Taveta Msaidizi Mkurugenzi wa Masuala wa masuala Mtambuka katika Baraza hilo Abdul-hakiim Machano Haji amesema wameanza kusafisha Barabara mbalimbali zilizomo katika Manispaa hiyo na kuondosha Majaa yasio rasmi ili kuepusha Maradhi ya Mripuko katika kipindi hiki cha Mvua za Masika. 

 Amesema wameshaanza kutoa elimu ya Mazingira katika Shehia mbalimbali za Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ ili Wananchi wazidi kupata uelewe na kudumisha kusafisha Mazingira. 

 Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema Baraza hilo linakabiliwa na tatizo la Upungufu wa Vifaa kama vile Gari za kubebea taka,Uhaba wa Vifaa vya kufanyia Usafi na Mwamko kwa baadhi ya Wanajamii katika suala la kudumusha Usafi wa Mazingira. 

 Kwa upande wake Diwani wa kuteuliwa Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ Thuwaiba Jeni Pandu ameahidi kufanya Ushawishi katika Baraza hilo ili kuhakikisha wanaongeza Bajeti katika mwaka 2020-2021 kwa ajili ya kununua Gari za kubebea Taka na Vifaa vya usafi na kuondokana na tatizo la Upungufu wa Vifaa katika Baraza hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.