Habari za Punde

Teknolojia Yawezesha Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa SADC Kufanyika Kuepuka COVID-19


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafisa Waandamizi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Balozi Kanali Wilbert Ibuge, akifungua mkutano wa maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakaofanyika Machi 18, 2020, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, JNICC Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafisa Waandamizi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Balozi Kanali Wilbert Ibuge, akiendesha  wa Maafisa Waandamizi SADC ambao ni maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakaofanyika Machi 18, 2020, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere, JNICC Jijini Dar es Salaam, Tanzania, kulia ni Katibu Mtendaji SADC’


Maafisa Waandamizi ambao pia ni Makatibu Wakuu wa Nchi mbalimbali za SADC wakifuatilia Mkutano wa Maafisa Waandamizi  unaofanyika kwa njia ya video conferencing ambo umefunguliwa leo Machi 17, 2020,JNICC Jijini Dar es Salaam, Tanzania 




Na. Mwandishi Wetu-MAELEZO                                                                                               
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafisa Waandamizi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Balozi Kanali Wilbert Ibuge amefungua kikao cha Maafisa Waandamizi chenye jukumu la kundaa ajenda za mkutano wa Baraza la Mawaziri utakaofanyika tarehe 18, Machi mwaka huu Jijini Dar es Salaam,Tanzania, ambacho kimefanyika kutokana na maendeleo ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA –ICT kwa nchi za SADC.

Akizungumza katika mkutano huo ambao unafanyika kwa Video Coferencing, Balozi Ibuge amesema kuwa kikao hicho kitajadili ajenda mbalimbali zikiwemo Taarifa ya Maandalizi ya Dira ya SADC ya mwaka 2050, Mpango Mkakati wa Maendeleo wa SADC 2020-2030, Maadhimisho ya miaka 40 ya SADC tangu kuanzishwa kwake mwaka 1980, Utekelezaji wa maazimio ya vikao vilivyopita, Hali ya michango na kifedha kwa ujumla ya SADC na Kupokea taarifa ya ukaguzi wa shughuli mbalimbali za Sekretariati ya SADC.

"Kikao hicho ambacho kinafanyika kwa njia ya Video Conferencing kufuatia ushauri uliotolewa na Mawaziri wa Afya wa Nchi za SADC walipofanya Mkutano wa dharura kufuatia mlipuko wa Ugonjwa wa Virusi vya Corona (Covid-19), uliofanyika Jijini Dar es Salaam Machi 9 2020, na tutakuwa na ajenda chache, nawasihi tuendelee kufuatilia na kutekeleza yale yote ambayo tumeyaazimia", amesema Balozi Ibuge.

Pamoja na hayo Balozi Ibuge amebainisha kuwa kuna uwezekano wa Maafisa Waandamizi wa Nchi hizo za ukanda wa Kusini Mwa Afrika (SADC),  kukutana mwezi Juni 2020 iwapo hali ya sasa ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona (Covid-19, itakuwa imebadilika ili kujadili kwa kina ajenda zilizosalia na zingine zitakazopendekezwa.

Mkutano huo ambao umeendeshwa kwa mara ya kwanza kwa kutumia njia ya Mtandao yaani Video conferencing kwa nchi za SADC, umethibitisha kukua kwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)-ICT na itaendelea kuimarishwa zaidi kwa Nchi hizi ili kuepuka kuwepo kwa taharuki ya milipuko mbalimbali au adha ambazo zitasababisha kuahirishwa kwa mikutano hiyo.

Aidha, amewataka wananchi wanachama kuendelea kuchukua tahadhari kujikinga na ugonjwa wa Corona ili kuepusha kusambaa katika nchi wanachama.

“Naomba nitumie fursa hii kuwaomba na kuwasihi nchi wanachama kuendelea kujinga na maambukizi ya Covid-19 na kushikamana kwa umoja wetu kupunguza kasi ya maambukizi na hatimaye kuondoa kabisa katika sura ya dunia”, Alisema Balozi Ibuge.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.