Habari za Punde

Wanawake Watakiwa Kucheki Afya Zao Mara kwa Mara.

Na. Takdir Suweid. Maelezo Zanzibar.
Wanawake nchini wametakiwa kupima afya mara kwa mara ili kujuwa maradhi yanayowakabili na kuyapatia matibabu kwa haraka.
Wito huo umetolewa na Katibu wa kikundi cha Zanzibar Mama’s Sharon Robert wakati wa zoezi la upimaji wa Afya kwa akinamama huko katika Hospitali Global Mnazimmoja.
Amesema bado Mwamko wa Wanawake katika kupima afya zao ni mdogo hivyo wameamua kupita nyumba hadi nyumba kutoa elimu ya Afya kwa akinamama.
Amesema iwapo watabaini Maradhi mapema watajuwa mbinu za kujikinga na kupata Matibabu ili maradhi yasizidi kuwaathiri.
Aidha ameziomba Taasisi binafsi kushirikiana na Serikali katika kuhamasisha Wananchi kushiriki kupima Afya zao ili kujuwa Afya zao na kuipunguzia Serikali mzigo mzito wa kusafirisha Wageni nje ya nchi.
Kwa upande wake Afisa uhusiano wa Hospitali ya Global Victoria Makanjuki amewataka akinamama kuangalia afya zao angalau kila baada ya miezi sita ili kupata uhakika na Mama bora katika familia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.