Habari za Punde

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Yawataka Wanafunzi Kutumia Muda Huu wa Likizo Waitumea Kwa Kujisomea.

Na Mwajuma Juma, Zanzibar
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imewataka Wanafunzi  wanaotarajiwa kufanya mitihani ya kidatu cha sita, kidatu na nne na kidatu cha pili  kutojibweteka katika  masomo yao na badala yake kundelea kujisomea ili kujiandaa vyema na mitihani yao.

Akitoa taarifa juu ya kufanyika kwa mitihani hiyo na uwepo wa maradhi ya korona, Mkugenzi Idara ya Elimu ya Sekondari Asya Iddi Issa amesema mitihani hiyo itafanyika kama kawaida kwa kulingana na hali ya maradhi hayo ikivyo hapa nchini.

Aidha  aliwataka wazazi, walezi na walimu kuhakikisha wanashirikiana kwa njia mbali mbali za mawasiliano katika suala la masomo kwa watoto ili kuwasaidia watoto katika kusoma na kuwaepuusha kurandaranda ovyo na kujibweteka katika katika masomo.

Alisema Wanafunzi wana fursa ya kutafuta msada wa masomo yao kupitia Maktaba kuu kwa kwenda kuazima vitabu na kujisomea nyumbani pamoja na kujipima kupitia katika mitihani iliopita ambayo inapatikana kwenye mtandao wa necta.

 Asya aliwataka wanafunzi kusoma na qur.ani wakati wanapokuwa nyumbani kutokana na kufungwa madrasa kutokana na maradhi hayo.

Alisema kufanya hivyo kutarahisisha watoto kutokuwa nyuma kielimu kwani kukaa bila ya kusoma kunaweza kuwafanya watoto kusahau wakichosomeshwa.

Aidha  aliwanasihi wazazi kutowaacha watoto kurandaranda ovyo mitaani na waendelee kubakia majumbani mwao na kufuata masharti yanayotolewa na Serikali juu ya maradhi hayo ili kuepukana na kuenea kwa maradhi hayo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.