Habari za Punde

Wafanyakazi Katika Bandari ya Mkjokotoni Watakiwa Kuchukua Tahadhari ya Kuchukua na Kupakia Abiria Katika Bandari Hiyo.


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif Mohamed akizungumza na Viongozi wa Bandari ya Mkokotoni, Manahodha na Wakuu wa Madiko kufuatia wimbi la uingiaji wa Watu usiozingatia utaratibu wa Banadari halali. Hapo ukuimbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini A Mkokotoni Unguja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Nd. Makame Khatib Makame akiwaasa Wafanyakazi wa Vyombo vya usafiri wa Baharini kuzingatia umuhimu wa kuwa na vifaa vya Maafa pamoja na vile vya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini katika Bandari ya Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja.Ndg. Pandu akielezea changa moto zinazowakabili Watendaji wa Mamlaka hiyo katika utendaji wa kazi zao ikiwemo ufinyu wa vifaa vya kazi.
Baadhi ya Viongozi wa Bandari ya Mkokotoni, Mkoa wa Kaskazini Unguja  Manahodha na Wakuu wa Madiko wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar hapo Mkokotoni Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya.

Na,Othman Khamis.OMPR.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ndg. Shaaban Seif  Mohamed amesema ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya Bandari Bubu hapa Nchini bado zinaendelea kutumiwa kwa kushushia Abiria kutoka Nje ya Zanzibar licha ya Agizo lililotolewa na Serikali Kuu kupiga marufuku suala hilo.

Alisema Agizo hilo la Serikali kamwe halijatenguliwa na kukumbusha kwamba vyombo vya Dola havitasita kuwachukuwa hatua za Kisheria Watu watakao kaidi Agizo hilo na kutaifisha Vyombo vyote vitakavyobainika kutumika katika kazi hiyo.

Ndg. Shaaban Seif Mohamed alieleza hayo katika Kikao cha pamoja kilichowakutanisha Viongozi na Watendaji wa Bandari ya Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakuu wa Madiko, Manahodha wa Vyombo vya Baharini, Viongozi wa Serikali ya Wilaya ya Kaskazini “A” Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo hapo Mkokotoni.

Kikao hicho kimekuja kufuatia ongezeko la baadhi ya Watu wanaoingia Zanzibar kwa kujipenyeza wakisingizia wanatoka Tanzania Bara kupitia Bandari Bubu ambao baadhi yao kwa uchunguzi wa Wataalamu wa Afya wamebainika kuwa na dalili za Virusi vya Corona.

Alisema kasi ya maambukizi ya Vizuri vya Corona inazidi kupanda na kutishia Maisha ya Wananchi hali inayoonekana baadhi ya Viongozi waliopewa dhamana kushindwa kutekeleza Majukumu yao kwa kuzingatia Zaidi muhali kutokana na wanaofanya vitendo hivyo wakiwa na ukaribu nao.

“ Visiwa vilikuwa na Wagonjwa wachache walioambukizwa Virusi vya Corona lakini kutokana na baadhi ya Viongozi kushindwa kutekeleza dhamana zao ongezeko la virusi hivyo linazidi kila kukicha”.

Alitanabahisha Ndg.Shaaban Seif.Katibu Mkuu huyo wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitahadharisha kwamba tabia ya dharau na kebehi inayofanywa na baadhi ya Watu yakutojali kuchukuwa tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona inaweza kuwa kama ni kuliangamiza Taifa ndani ya kipindi kifupi.

Alisema tabia hii yahatari inaiongezea mzigo Serikali Kuu wakati huu ambao Sekta ya Utalii na Biashara zinazoliingizia mapato Taifa zimesita kufanyakazi kutokana na janga hili la Virusi hivyo ambavyo hadi muda huu bado halijapatiwa tiba sahihi la kukabiliana nalo.

Amewakumbusha Viongozi na wasimamizi wa Bandari ya Mkokotoni kuendelea kutoa huduma huku wakizingatia kwamba Bandari hiyo imepata Baraka ya kutoa huduma za upakizi na upakuaji wa mizigo pekee na sio kupitisha Abiria kama inavyofanywa katika muda mwingi sasa.

Alisema dhamira ya Serikali ni kuwarahisishia Wananchi na Wafanyabiashara kupunguza mzunguko wa upatikanaji wa bidhaa zinazohitajika ndani ya Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa zile zinazotoka katika Mkoa wa Tanga Tanzania Bara.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Ndg. Makame Khatibu Makame alisema baadhi ya vyombo vya usafiri wa Baharini bado havijazingatia umuhimu wa kuwana vifaa vya maafa sambamba na vile vya kujilinda na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Ndg. Makame alisema hali hiyo inaweza kwa kiasi kikubwa kuambukiza kwa haraka Virusi hivyo kutokana na msongamano wa abiria katika vyombo hivyo licha ya kuonywa kuchukuwa kawaida na kukabalika kwa mujibu wa usajili wa chombo husika.

Wakichangia katika Kikao hicho baadhi ya Viongozi na watendaji wa Taasisi zilizo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “A”Unguja walieleza changamoto kubwa inayowakabilini ukosefu wa vifaa vya kutekeleza majukumu yao ya kila siku hasa kipindi hichi cha mripuko wa janga la Virusi vya Corona.

Walisema ukosefu wa boti za Doria pamoja na gari za kufuatilia matukio pale yanaporipotiwa hasa kipindi hichi cha uingiaji wa watu kutoka nje ya Zanzibar ni changamoto kubwa inayopaswa kuchukuliwa hatua za dharura na Serikali pamoja na Taasisi za kielimu kupunguza changamoto hizo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.