Habari za Punde

Mamia Wajitokeza Maziko ya Mtoto wa Sokoine : Alazaro Sokoine Azikwa Leo

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo ameongoza watumishi wa Ofisi yake katika mazishi ya Alazaro Sokoine ambaye ni mtoto Mkubwa wa Hayati Edward Moringe Sokoine. Mazishi hayo yamefanyika jana Monduli Juu Mkoani Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, ndugu, jamaa na Marafiki.
Mkurugenzi wa Utawala na usimamizi wa Rasilimali watu Bi. Emma Lyimo akitoa heshima za mwisho katika ibaada ya kuaga mwili wa Alazaro Sokoine ambae ni mtoto mkubwa wa Hayati Edward Moringe Sokoine. Mazishi yamefanyika jana Monduli Mkoani Arusha.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine (kushoto) akiweka shada la maua pamoja wanafamilia katika kaburi la kaka yake mkubwa Alazaro Sokoine. Mazishi yamefanyika jana Monduli Mkoani Arusha. 

Wakuu wa Mikoa ya Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka, Morogogo - Mhe. Loata Sanare, Tanga - Mhe. Martine Shigela na Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakiweka shada la maua katika kaburi la Alazaro Sokoine, Monduli Mkoani Arusha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.