Habari za Punde

Mvua za masika zaleta athari katika maeneo ya mji wa Zanzibar

 MVUA za Masika zinazoendelea kunyesha, wakaazi wa mtaa wa Mwera nyuma ya Kituo cha Poilisi wamejipatia ajira ya kuvusha wakaazi wa mtaa wa huo kutokana na daraja la kuvukia kwenda mtaa wa pili kufunikwa na maji ya mvua.
 BAADHI ya wakaazi wa mtaa wa Mwera nyuma ya Kituo cha Polisi wakivuka daraja lililofunikwa na maji ya mvua za masika zinazoendelea kunyesha kwa siku ya pili mfululizo.
 WAYA za umeme ambazo zimeunganishwa na Tranfoma, mtaa wa Mwera nyuma ya Kituo cha Polisi, zikiwa karibu sana kuingiwa na maji ya mvua ambayo tayari yameshalifunika daraja la linalotimika na wakaazi wa mta huo, huku baadhi ya wananchi hulazimisha kuvuka kwenda katika makaazi yao.
 MVUA za Masika zinazoendelea kunyesha, zimeanza kuleta athari, katika mitaa ya Jango’mbe baadhi ya nyumba tayari zikiwa zimeingiwa na maji ya mvua hizo. 
WANANCHI wakiwa wanatoa maji katika nyumba yao kwa kutumia jenereta kama walivyokutwa na mpiga picha mitaa ya Mwera Regeza Mwendo (PICHA ZOTE NA ABDALLA OMAR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.