Habari za Punde

Virusi vya Corona: Papa awataka watu 'kutokubali kushindwa na uoga'

Papa Francis amewataka watu kutosalimu amri kwa uoga wa virusi vya corona, na kuwataka kuwa "wajumbe wa uhai wakati wa kifo".
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki alizungumza wakati wa sherehe za pasaka Jumamosi, katika kanisa la St Peter's Basilica ambalo lilikuwa na watu wachache.
Waumini wa Kikatoliki bilioni 1.3 kote duniani wana fursa ya kufuatilia ibada ya moja kwa moja mtandaoni.
Marufuku ya watu kutokutoka majumbani bado inaendelezwa katika maeneo mbalimbali nchini Italia ambako kumeathiriwa vibata na janga la Corona.
Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte alimsifu Papa kwa kuonyesha kuchukua majukumu yake kwa tahadhari baada ya kuadhimisha ibada ya pasaka bila ya mkusanyiko wa waumini.
Wakristo kote duniani wanasherehekea sikukuu ya pasaka, moja ya sikukuu muhimu katika kalenda ya Kikikristo licha ya hatua zilizochukuliwa katika nchi nyingi duniani zilizosababisha mamilioni ya watu kusalia majumbani
Makasisi wengi wanaendesha ibada zao makanisani bila waumini kukusanyika.
Papa Francis alirejelelea maandiko ya bibilia kuhusu mwanamke ambaye hakumkuta hata mtu mmoja katika kaburi la Yesu siku ambayo Wakristo wanaamini alifufuka.
"Wakati huo pia, kulikuwa na hofu ya siku zijazo na kwamba kutakuwa na haja ya kuanza upya. Kumbukumbu ya huzuni, na kukatizwa kwa matumaini. Kwao, kama ilivyo kwetu, ilikuwa saa ya giza," Papa amesema.
"Msiwe na hofu wala msiogope: Huu ni ujumbe wa matumaini. Tumeupokea leo hii," aliongeza.
Ibada yake, ambayo kawaida hufanyika mbele ya maelfu ya waumini, ilihudhuriwa na watu kumi na kitu tu. Tamaduni kadhaa za ibada za kanisa hilo pia hazikufanyika ikiwemo ubatizo wa watu waliobadili dini a kuingia katika Ukatoliki.
Papa anatarajiwa kutoa ujumbe wake wa Jumapili ya pasaka katika sherehe ambayo haitahudhuriwa na watu. Kihistoria, ujumbe wa siku kama ya leo umekuwa ukitolewa mbele ya watu wengi katika uwanja wa katina la Mtakatifu Petro.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.