Habari za Punde

THBUB Wawapongeza Wauguzi Hospitali ya Mkoa Dodoma Kuadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani.

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Dkt. Fatma Rashid Khalfani (kushoto) akikabidhi zawadi ya Keki kwa Mkurugenzi wa Wauguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Stanley Mahundo (kulia) ikiwa ni ishara ya kuwapongeza Wauguzi kwa kazi nzuri wanayoifanya. Pamoja na keki hiyo, Dkt. Fatma alikabidhi pia sabuni kwa ajili ya Wauguzi hao kuzitumia kunawia mikono kwa ajili ya kujikinga na Korona.
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Dkt. Fatma Rashid Khalfani (Kulia) akiongea na Mkurugenzi wa Wauguzi katika Hospitali ya Mkoa Dodoma, Stanley Mahundo alipomtembelea Hospitali hiyo kwa lengo la kuwapongeza Wauguzi kuelekea maadhimisho ya Siku ya wauguzi duniani inayosheherekewa  Mei 12 ya kila Mwaka. 
Sister Fidence, MC, Mkuu  wa Kituo cha kutunza Watoto na Wazee cha Home of Joy and Love Kilichopo Hombolo jijini Dodoma akimtembeza Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Dkt. Fatma Rashid Khalfani (kulia) kumuonesha maeneo mbalimbali ya kituo hicho Mei 11, 2020. Ziara hiyo ya Kamishna ilikuwa na lengo la kutoa elimu ya haki ya afya ili kuwahamasisha kuendelea kuzingatia maelekezo yanayotolewa ya kujikinga na maradhi ya Korona. Kushoto ni Afisa wa THBUB, Fides Shayo.

Mkuu  wa Kituo cha kutunza Watoto na Wazee cha Home of Joy and Love kilichopo Hombolo, Dodoma, Sister Fidence MC (kulia) akimuonesha Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Dkt. Fatma Rashid Khalfani (katikati) mabweni wanayokaa Watoto  alipotembelea kituo hicho Mei 11, 2020. Kushoto ni Afisa wa THBUB, Fides Shayo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.