Habari za Punde

Uongozi wa Klabu ya Negro United Wasibiria Kuendelea Kwa Ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini.


NA MWAJUMA JUMA
KATIBU wa timu ya soka ya Negro United  Mbaraka Abdalla amesema kuwa anasikiliza kauli ya viongozi wao kuhusu kuendelea ligi ili na wao waweze kuanza mazoezi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema kuwa wao hawana maneno yoyote na kitakachoamuliwa ndicho watakachokifata.

“Tumekaa tunasubiri kauli ya viongozi wetu wakituambia ligi ipo tutafata na kama haipo pia”, alisema Katibu huyo.

Hata hivyo alisema kuwa wao kama viongozi wanaendelea kuwafahamisha wachezaji wao namna ya kujikinga na maradhi ya Corona ili waweze kuwa salama.

Alisema kuwa janga hili ni kubwa kwa dunia nzima na kwa vile mikusanyiko imekatazwa inawabidi wafate maelekezo ya wataalamu ili kuwa salama.

Negro United inashiriki ligi daraja la pili wilaya ya Mjini ambapo hadi ligi hiyo inasimama inaongoza kundi B ikiwa na pointi 26 na inafatiwa na Sebleni United wenye pointi 25.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.