Habari za Punde

Katibu Mkuu Ndg.Nzunda Akagua Maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda pamoja na timu aliyoongozana nayo wakiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Tume ya Uchaguzi (NEC) lililopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma.
Mhandisi wa mifumo ya zima moto, Gaudence Kessy akitoa ufafanuzi wa hatua za ufungaji wa mifumo hiyo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda wakati wa ziara hiyo
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda akitoa maelekezo kwa Msimamizi na Meneja wa Mradi wa Ujenzi kutoka Chuo kikuu cha Ardhi, Godwin Maro wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) lililopo eneo la Njedengwa Dodoma Juni 18, 2020 unaosimamiwa na Kikosi cha SUMA JKT.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda akitoa majumuisho ya ziara yake katika Jengo la NEC kwa timu inayosimamia ujenzi huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.