Habari za Punde

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MAHANDAKI YATAKAYOPITISHA TRENI YA KISASA YA UMEME STANDARD GAUGE SGR KILOSA MKOANI MOROGORO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Eng. IsackKamwelwe pamoja na viongozi mbalimbali akiweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Mahandaki ya Reli yatakayopitisha Treni ya Kisasa ya Umeme Standard Gauge katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Mahandaki ya Reli yatakayopitisha Treni ya Umeme Standard Gauge katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Eng. IsackKamwelwe pamoja na viongozi mbalimbali akiweka jiwe la msingi Ujenzi wa Barabara ya Dumila-Kilosa-Mikumi sehemu ya Rudewa-Kilosa Km 24 katika sherehe zilizofanyika katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na baadhi ya Mawaziri, wakuu wa Mikoa,viongozi mbalimbali, akikata utepe ili kuzindua mitamboitakayotumika katika ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro.
Sehemu ya Handaki kubwa lenye urefu wa Kilometa 1.1 ambalo litapitishatreni hiyo katika eneo la milima ya Kilosa mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipitandani ya Handaki kubwa lenye urefu wa kilometa 1.1 kulikagua mara baada ya kuweka jiwe la msingi la miradi hiyo ya ujenzi Kilosa mkoani Morogoro.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mawaziri, baadhi ya Viongozi wa Serikali, katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kampunizinazojenga mradi wa Reli ya Kisasa SGR Kilosa mkoani Morogoro.
PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.