Habari za Punde

RC Kusini awaapisha Masheha aliowateua karibuni

Na Madina Issa

MKUU wa Mkoa wa kusini Unguja, Ayoub Mohammed Mahmoud, amewaapisha masheha 21 aliyewateuwa hivi karibuni kutumikia nafasi hiyo kati ya masheha 22.
Akizungumza mara baada ya kuwaapisha Mkuu wa Mkoa huyo, alisema ametengua uteuzi wa sheha wa shehia ya Ndijani Mseweni, Khatib Mtumweni Khatib kutokana na kudai kuwa akija kuapa kiapo cha sheha atarogwa.
“Natengua kwa kuwa sheha huyo, amekosa uzalendo na nitachagua sheha mwengine ili azibe nafasi hii na kama sote tunaogopa kurogwa taifa lisingekuwa hivi hivyo, masheha tufanyeni kazi kwa mujibu wa sheria zetu za nchi” alisema.
Alisema masheha ndio wenye dhamana katika shehia, hivyo aliwataka kuendelea kufuata sheria, Maadili na Kanuni watakazokabidhiwa zinatumika wa kuwatumikia wananchi wa shehia zao.
Hivyo, aliwataka masheha hao kutojihusisha katika migogoro ya ardhi, na kuwakumbusha kuendelea kuiheshimu sheria ya nchi ili wasishirikishwe katika migogoro hiyo.
Alisema kwa mujibu wa sheria namba 8 ya mwaka 2014 kifungu cha 27 kifungu kidogo cha 4 ambapo kinaeleza wazi sheha atakayeteuliwa na mkuu wa mkoa hatofanya majuku yake bila ya kuapishwa.

Sambamba na hayo, aliwataka masheha hao kuheshimu mali za watu, ambapo kwa mujibu wa masheha ni kuwatumikia wananchi kwani kazi ya kuwahudumia wananchi sio kazi nyepesi hivyo waendelee kujitahidi kufanya kazi kwa mujibu wa sheria.

Waliyoapishwa kwa upande wa wilaya ya kati walikuwa 15, Bishara Saleh Haji Shehia ya Kidimni, Makame Simai Makame shehia ya Pagali, Aziza Juma Mtumwa, shehia ya Tunduni, Karim Ali Haji shehia ya Ndijani muembe punda, Zidi Suleiman Abjedi shehia ya Jendele.
Wengine ni Hassan Makame Haji shehia ya Ukongoroni, Simai Haji Makame, Unguja Ukuu Tindini, Issa Haji Makame,sheha wa Ghana na Idd Ramadhan Choum sheha wa shehia ya Tunguu.
Akiwataja wengine ni Kondo Mwadini Kondo  shehia ya  dunga bweni, Juma hamza abasi shehia ya marumbi, Adam muhsini amour  shehia ya uroa, Abdalla juma salum  machui na pandu hassan pandu shehia ya ubago.
Kwa upande wa masheha walioteuliwa upande wa kusini, rashid ali hassan shehia ya kizimkazi mkunguni,  Hassan Amour Alu shehia ya Muyuni ‘C’, Mohd Rajab Makame shehia ya Paje
Mussa Juma Mbwato shehia ya Muungoni, Maryamu Pandu Kweleza shehia ya Bwejuu, Ali Khatib Pandu shehia ya Muyuni ‘A’ na Hassan Fadhil Suleiman shehia ya Nganani.

Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika hafla hiyo ni mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa kusini Unguja, Ramadhan Abdallah Ali (Kichupa), wakuu wa wilaya ya ya kati na Kusini Unguja

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.