Habari za Punde

RITA IMEANZA KUDHIBITI CHANGAMOTO YA USAJILI WA VYETI NCHINI

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari akifungua kikao cha hamasa kwa viongozi wa mkoa na wilaya zake kuhusu usajili wa watoto walio na umri chini ya miaka mitano juzi kilichoandaliwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) na kufanyika katika ukimbi wa mkuu wa mkoa Tanga.
Picha na : Hamida Kamchalla
Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini Emmy Hudson, akizungumza wakati wa hafla ya Kikao cha hamasa kwa Viongozi wa Mkoa na Wilaya  kuhusiana na mpango wa usajili wa Watoto walioko chini ya umri wa miaka mitano uliofanyika katika ukumbiu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Na Hamida Kamchalla, TANGA.
KUTOKANA na ongezeko la mahitaji na matumizi ya cheti cha kuzaliwa nchini, hali ya usajili na utunzaji wa kumbukumbu ya vizazi bado hairidhishi jambo linalosababisha serikali kukosa takwimu sahihi kwa ajili ya mipango mbalimbali ya maendeleo.

Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini Emmy Hudson ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa kikao cha hamasa kwa viongozi wa mkoa na wilaya zake kuhusu mpango wa usajili wa watoto walio na umri chini ya miaka Kitano kilichofanyika katika ukumbi wa jengo la mkuu wa mkoa wa Tanga.

Hudson ameeleza kwamba kutokana na halo hiyo serikali inashindwa kutoa huduma za maendeleo kwa Taifa nabutoaji wa huduma za jamii kama vile Afya, Elimu na huduma nyingine za msingi.

Aidha amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu ya sensa ya 2012 ni asilimia 13 tu ya wananchi wa Tanzania Bara walisajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa hivyo kuifanya kuwa moja kati ya nchi zenye kiwango cha chini cha usajili barani Afrika.

"Hii ni changamoto ambayo serikali kupitia RITA kama Taasisi yenye dhamana ya Usajili wa matukio muhimu ya binadamu kwa kwa kushirikiana na wadau wengine tumechukua hatua stahiki kwa kuandaa mkakati wenye lengo la kukabiliana na changamoto hii" amesema Hudaon.

Hata hivyo amebainisha kwamba tayari hatua madhubuti zimechukuliwa ili kukabiliana na changamoto hiyo kwa kufanya maboresho ya ujumla ya mfumo mzima wa usajili chini ya mkakayi wa Kitaifa na kuboresha Usajili wa matukio muhimu ya binadamu na takwimu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.