Habari za Punde

Waziri Mahmoud Azungumza na Balozi wa Itali Nchini Tanzania

Waziri wa Habari ,Utalii na Mambo ya kale  Zanzibar Mhe.Mahmoud Thabit Kombo akisisistiza kwa  waandishi wa habari alipotembelewa na Balozi wa Italy ,huko ukumbi wa Wizara ya habari Kikwajuni Zanzibar. .
Balozi wa Italy nchini Tanzania Robert Mangoni akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujaji wa  watalii kipindi hiki cha mripuko wa maradhi ya Corona ,huko Kikwajuni katika  ukumbi wa Wizara ya habari  Zanzibar.
Waziri wa Habari ,Utalii na Mambo ya kale Mahmoud Thabit Kombo akionyesha muongozo wa uendeshaji Utalii Zanzibar katika kipindi cha COVID-19,hafla iliyofanyika  ukumbi wa Wizara ya habari Kikwajuni Zanzibar. 
Picha na Fauzia Mussa - Maelezo Zanzibar.

Na.Issa Mzee, Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mhe Mahmoud Thabit Kombo amefanya mazunguzo na Balozi wa Itali nchini Tanzania ili kuurejesha utalii na kukuza uchumi Zanzibar.
Akizungumza na Balozi huyo ofisi kwake Kikwajuni Zanzibar amesema Italy ni mdau mkuu wa kuleta watalii ukilinganisha na mataifa mengine ya Ulaya kutokana na uwekezaji mkubwa waliofanya nchini.
Amesema lengo kuu ni kurejesha soko la watalii wa Itali Zanzibar baada kufunguliwa milango ya utalii visiwani hapa ili kuinua uchumi wa zanzibar ambao umeathiriwa vibaya na maradhi ya corona.
“Tumefanya majadiliano na Balozi huyu kuhusu namna ya kuresha tena wageni wao kuja Zanzibar ikwemo namna ya kurejesha ndege za kitalii na kuja kujionea hali halisi ya usalama wa maeneo ya kitalii ilivyo Zanzibar”.alisema Waziri
Aidha alifafanua kuwa bado utaratibu wa kuwapima afya bado unaendela na yeyote atakegundulika na dalili za corona taratibu za afya zitafuata ili kuwaweka salama wananchi dhidi ya ugonjwa huo.
Kwa upande wake Balozi wa Italy nchini Tanzania Bw Roberto Mengoni ameipongeza serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jitihada zilizochukuliwa ili kudhibti ugonjwa wa corona na kufungua tena milango ya utalii nchini.
“Nimetembelea maeneo mbalimbali ya kitalii ikiwemo mahoteli,sehemu za fukwe na baadhi ya vituo vya afya ili kuhakikisha usalama wa raia wetu watakao kuja Zanzibar” alisema Balozi.
Amesema Zanzibar ni kituo muhimu kiutalii kwa raia wa Italy hivyo amekuja  kukagua na kuhakikisha kwamba raia wao wanakuwa salama wapoingia 

1 comment:

  1. Ushauri tu, hao watalii kama hawajafanya safari ya kuja Tanzania wafanye checking ya covid19 huko huko kwao na wapate cheti cha uthibitisho, utaratibu huu sasa watumika Dubai

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.