Habari za Punde

Mgombea Urais wa Zanzibar Kupitia Chama Cha Mapinduzi Mhe Hussein Mwinyi Achukua Fomu leo Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Hussein Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Wananchi na WanaCCM alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui baada ya kukamilisha zoezi la Uchukuaji wa Fomu Ofisi za Tume ya Uchaguzi Maisara Jijini Zanzibar leo 26/8/2020 na kuzungumza na Wanachama wa CCM katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibare (ZEC) Mhe. Jaji Mkuu Mstaaf Hamid Mahmoud Hamid akimkabidhi Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Mhe. Hussein Ali Hassan Mwinyi, alipofika Ofisi za Tume Maisara Jijini Zanzibar kwa uchukuaji wa Fomu leo 26/8/2020. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe Hussein Ali Hassan Mwinyi akiwaonesha Mkoba ukiwa na Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar, baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mhe. Jaji Mkuu Mstaaf wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Cham,a Cha Mapinduzi Mhe. Hussein Ali Hassan Mwinyi akiwa na Mkewe, baada ya kukabidhiwa Fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar. hafla hiyo imefanyika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Maisara Jijini Zanzibar leo 26/8/2020.  
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe. Jaji Mkuu Mstaaf wa Zanzibar Hamif Mahmoud Hamid akizungumza kabla ya kuaza kwa zoezi la kutowa Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar kwa Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Mhe Hussein Mwinyi, hafla hiyto imefanyika leo katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Maisara Jijini Zanzibar.

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe Hussein Mwinyi akiangalia ngoma ya kibati alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar baada ya kumaliza hafla ya uchukuaji wa Fomu ya Urais Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitria Chama Cha Mapinduzi Mhe,Hussein Mwinyi akiwapongia mkono Wananchi wakati akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui akitoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) baada ya kumaliza zoezi la uchukuaji wa Fomu leo.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.