Habari za Punde

World Vision Yatumia Shilingi Bilioni 12.7 Katika Miradi Mbalimbali ya Maendeleo.

Mgeni rasmi Katibu tawala wilaya ya Bukoba Kadore Kilugala akihutubia kwaniaba ya mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro kwenye hafla ya kufunga mradi wa Katerero AP.
Mkurugenzi wa miradi wa shirika la World Vision Tanzania akitoa taarifa ya mradi wa Katerero AP kwa mgeni rasmi pamoja na wananchi waliojitokeza kwenye hafla ya kuufunga mradi huo.  
Mratibu wa mradi wa Katerero AP Atugonza Kyaruzi akitoa ufafanuzi wa namna wananchi walivyonufaika na mradi wa Katerero AP Kwa wananchi na Mgeni Rasmi.
Wanavikundi walionufaika na mradi wa Katerero AP Wakimuonyesha baadhi ya bidhaa mgeni Rasmi wanazoshughulika nazo baada ya kusaidiwa na shirika la World Vision.
Wanafunzi wa shule ya msingi Katerero wakitoa burudani kwenye hafla ya kufunga mradi wa Katerero AP unaofadhiliwa na shirika la World Vision Tanzania.

Na Allawi Kaboyo Bukoba
Shirika lisilo la kiserikali la World Vision Tanzania limetumia Zaidi ya shilingi Bilion 12 kwa miaka 17 kuendesha miradi mbalimbali katika mradi wao mkuu uliojulikana kama Kaerero AP halmashauri ya wilaya Bukoba mkoani Kagera Kwa kuwanufaisha wananchi 28,671

Akiongea katika hafla ya kuufunga mradi huo iliyofanyika Agost 26, mwaka huu na kuhudhuliwa na Katibu tawala wa wilaya ya Bukoba Kadole Kilugala aliyekuja kwaniaba ya mkuu wa wilaya hiyo pamoja na baadhi ya wananchi wanufaika wa mradi Mkurugenzi wa miradi shirika la world vi­sion Tanzania John Masenza alisema,mradi wa kata Katerero um­eweza kuhudumia viji­ji 10 na kata nne amb­apo umenufaisha watu 39090 huku wanufaika wa moja kwa moja wakiwa 28,671.

Masenza alisema,wanu­faika hapa wameweza kujifunza shughuli za kilimo, ufugaji ,ujasiriamali, ubores­haji wa afya maji na elimu na kugarimu shilingi bilioni 12.7 kwa muda wa miaka 17 ya mradi huo.

Hata hivyo alisema kuonekana kwa mafanik­io hayo ni kwa ushir­ikiano wa Serikali na shirika kwa ufadh­ili wa nchi ya Aust­ralia iliyokuwa ikit­oa pesa ya huduma hi­zo.

Katibu Tawala wa wil­aya Bukoba Kadole Ki­lugala alisema,ujuzi uliojengwa kwa wana­nchi wa kata nne nda­ni ya wilaya hiyo,it­asaidia kuwafaa kipi­ndi chote ambacho sh­irika halitakuwepo.

"Tambueni mtu anaeku­pa ujuzi wa Jambo la kujitegemea Ni mzuri kuliko yule anayekupa leo alafu kesho usim­wone tena niwaambieni ujuzi huu utumieni nyakati zote shirika linapokuwa halipo"­alisema Kilugala

Vile vile Kilugala alisema, mashirika ya­nayoleta ufadhili kwa jamii yanasaidia kuongeza msukumo wa maendeleo kwani yanaw­eka mchango wake kwa Serikali kusaidia jamii ambayo inauhita­ji muhimu.,

BAADHI ya Wananchi wa kata katerero wil­aya ya Bukoba mkoani Kagera wameiomba Se­rikali kuwapatia ufa­hamu wa jinsi ya kue­ndesha miradi ya mae­ndeleo kwa jamii inayoanzishwa na Serikali pamoja na wafadhiri mbalimbali ili kuleta matokeo cha­nya yatokanayo na miradi hiyo.

Walisema ufahamu huo utasaidia kuongeza  sehemu ya kuelewa shughuli inayoletwa kwa jamii Kama namna ya kusaidia katika uzalishaji mali ndani ya  sekta mba­limbali ambapo mradi huo ulikuwa ukihudumu kwenye kata za Katerero,Bujugo, Kanyangereko na Kemondo.

Johanes Joel mkazi wa kata Katerero alis­ema, miradi inayolet­wa inawalenga wananc­hi kuwabadilisha kwe­nye maisha na kupiga hatua ya maendeleo kwa kile kinachokusu­diwa.
"Bila kupewa kwanza ufahamu inakuwa vigu­mu kuyafanya na kuon­yesha mwitikio kwani hatuna mwanga wa ku­endesha wenyewe na kupata kitu chanya"al­isema Joel

Jeneroza Hamlungi mk­azi wa kijiji Burinda kata Bujugo alisema,kuwa na wingi wa miradi inategemewa wananchi kupewa elimu ya kuf­ahamu jambo na kutoka kwenye utegemezi wa ndugu na Serikali.

Aidha alisema idadi kubwa mashirika yana­toa elimu wezeshi kwa jamii kabla ya kuw­apatia mradi na huka­kikisha kundi linasi­mama lenyewe na kunu­faika Kama wanavyote­gemea .

"Jamii inamwitikio endapo itatambua kile kinacholetwa kinahi­taji nini kwa Jami na kufundisha na kufi­kia wengine wengine kutoa kwenye umasiki­ni mi napongeza mash­irika "alisema Hamlu­ngi.
  
Sharifa Kakulwa mwen­yekiti wa Kamati ya maendeleo ya Jamii kata Katerero alisema kupitia shirika la world vision wananchi wameweza kuunda vi­kundi zaidi ya 300 am­bavyo vinanufaika na uchumi, kilimo,afya, elimu, maji.

Aliongeza kuwa,kundi la wanawake limeamka na kujiamini kuanz­isha uzalishaji ambao unawapatia kipato na kuendesha maisha yao tofauti na hapo awali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.