Habari za Punde

CCM BIHARAMULO YAVUNJA REKODI UZINDUZI WA KAMPEINI, WATIA NIA ZAIDI YA 50 WALIOKATWA WAJITOKEZA KUNADI MTEULIWA.

Mgombea ubunge wa CCM jimbo la Biharamulo Mhandisi Ezra John Chiwelesa akihutubia mamia ya wananchi wa wilaya hiyo waliojitokezamkwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeini wilayani humo septemba 11, mwaka huu.
Mjumbe wa NEC kutoka mkoa wa Kagera na mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampein wilayani Biharamulo Mhe. Wilbroud Mutabuzi Kushoto akimpatia mkono mgombea ubunghe jimbo la Biharamulo Eng.Ezra Chiwelesa kulia baada ya kumkabidhi ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2020-2025 Kwaajili ya kuinadi kwa wanannchi wa Biharamulo.
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Biharamulo Mhe.Oscar Mkasa akiomba kura za CCM kwa wanabiharamulo kwa kuwaomba wamchague Rais Magufuli, Mbunge Ezra na Madiwani wote wa CCM.
Mke wa mgombea Ubunge jimbo la Biharamulo Bi, Exelia Ezra akimuombea kura mume wake ambaye ni mgombea ubunge kwa kupiga magoti ikiwa ni ishara ya heshima na unyeyekevu kwa wanabiharamulo.
Muonekano wa ummati wa wanabiharamulo walivyojitokeza kwa wingi katika mkutano wa ufunguzi wa Kampeini za CCM wilayani humo kwaajili ya kusikiliza sera zitakazowapelekea kukichagua chama hicho kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28,mwaka huu.

Na Allawi Kaboyo Biharamulo.
Vyama vya siasa vikiwa katika harakati za kuomba ridhaa ya wananchi ya kuchaguliwa kuongoza nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu ujao hapa nchini, Chama cha mapinduzi wilayani Biharamulo Mkoani Kagera kimeweka mikakati kabambe ambayo itawafanya wananchi wakichague katika nafasi za udiwani ubunge na urais kwa kura za kishindo
Chama hicho  kimezindua kampeni zake rasmi wilayani humo septemba 11, mwaka huu katika uwanja wa mpira wa ccm uliopo Biharamulo mjini, kwa kuahidi kuendelea kuboresha miundombinu na kuboresha huduma za kijamii huku mgombea ubunge kupitia chama hicho mhandisi Ezra John Chiwelesa akiahidi kutekeleza ilani ya chama chake na vipaumbele vyake vinne kwa wanabiharamulo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara, mgombea ubunge huyo aliyeteuliwa na chama chake kuipeperusha bendera amesema kuwa endapo wananchi wa jimbo hilo watampatia ridhaa ya kuongoza jimbo hilo kwa miaka mitano atahakikisha anaboresha huduma za afya hasa upande wa kinamama wajawazito, Miundombinu ya shule, Maji na kwakushirikiana na wananchi wa wilaya hiyo kutatua changamoto sugu zilizowasumbua kwa kipindi kirefu.
“Mimi nimezaliwa na kusomea hapa elimju yangu ya msingi mama yangu alikuwa akiuza nyanya sokoni kunisomesha Maisha ya wanabiharamulo nayajua sana ndiomaana nimeamua kuja kutumia elimu na maarifa yangu ya uhandisi kwa mustakabali wa wananchi na ndugu zangu wa Biharamulo, serikali yetu chini ya jemedari wetu Dkt,John Magufuli imefanya mambo makubwa na yanaonekana hivyo naomba ridhaa ya miaka mitano ili kuweza kuyaendeleza haya yaliyoletwa kwetu,” Amesema Mhandisi Ezra Chiwelesa.
Kufatia kuwepo kwa migogoro mbalimbali ya ardhi na mirathi wilayani humo, mgombea huyo amesema kuwa akichaguliwa atawaajili wanasheria kwaajili ya kutoa msaada wa kisheria bure kwa wananchi wa Biharamulo, huku akiahidi kuboresha sekta ya michezo kwa vijana na kuibua vipaji kwa kuanzisha Biharamulo star search.
Katika kutekeleza ilani Ezra amesema kuwa ilani ya uchaguzi yam waka 2020-2025 imeweka bayana ujenzi wa barabara ya nyakanazi Benaco ambayo imekuwa kero kwa kipindi kirefu kuwa itatengenezwa kwa kiwango cha lami ili kuweza kupitika kwa urahisi na kupunguza uharibifu wa vyombo vya moto.
Wakiongea kwa nyakati tofauti waliokuwa watia nia wenzaka katika kura za maoni wamesema kuwa kwasasa wameamua kuungana na kuwa kitu mimoja kwa kuhakikisha chama chao kinashinda kwa kura nyingi za urai, ubunge na madiwani ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa Biharamulo.
Oscar mkasa ni mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo hilo, katika kumuombea kura mgombea kwaniaba ya wenzake,amesema kuwa chama chao ni chama chenye demokrasia hivyo kiliamua kumleta Ezra kwaajili ya kuinua maendeleo ya wananchi wa Biharamulo ili kuweza kuendeleza pale alipoishia yeye, huku akiahidi kuendelea kumuunga mkono na kuhakikisha anashinda kwa kishindo.
Hata hivyo mkutano huo umewakutanisha viongozi mbalimbali wa chama hicho ambapo mbunge mteule viti maalumu mkoa wa Kagera kupitia jumuiya yay a UWT Regina Zachwa ametumia jukwaa hilo kukiombea kura chama chake kwa kuwaomba wanabiharamulo kumchagua Rais Magufuli kwa kura nyingi lakini kumchagua Ezra kwa maendeleo ya Biharamulo pamoja na madiwani wote wa kata 17 za wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.