Habari za Punde

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein Amnadi Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Mwinyi Katika Mkutano wa Kampeni Gando Pemba.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwahutubia Wananchi na WanaChama wa CCM wa Wilaya ya Wete Pemba katika mkutano wa kampeni ya kumnadi Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe.Dk.Hussein Mwinyi uliofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Gando Wete Pemba leo 27-9-2020. na kuwaobea Kura Wabunge, Wawakilishi na Madiwani wa CCM. 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Ubunge wa Majimbo ya Wilaya ya Wete Pemba wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar uliofanyika katika uwanja wa mpira Gando Pemba.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Gando Pemba Ndg. Salim Mussa Omar akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni ya CCM uliofanyika katika uwanja wa Gando Wete na kuwaombea Kura Wagombea Ubunge na Uwakilishi na Madiuwani wa Wilaya ya Wete Pemba katika mkutano wa kampenin ya Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Mwinyi.
Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Pemba na wakifutilia mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe. Hussein Ali Hassan Mwinyi uliofanyika katika uwanja wa mpira Gando Wilaya ya Wete Pemba.
Mwanachama wa Chama cha ACT -Wazalendo Bi, Rahma Shehe Hamad akionesha kadi yake ya ACT -Wazalendo baada ya kutangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Mwinyi uliofanyika uwanja wa mpira Gando Wilaya ya Wete Pemba.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza aliyekuwa Mwanachama wa ACT-Wazalendo Bi. Rahma Shehe Hamad, akitangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Mwinyi uliofanyika katika uwanja wa Gando Wilaya ya Wete Pemba.  
Waziri Kiongozi Mstaaf wa Zanzibar Mhe. Shamsi Vuai Nahodha akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe.Dk. Hussein Mwinyi, na kumuombea Kura kwa Wananchi wa Pemba na kuwaombea kura Wabunge, Wawakilishi na Madiwani wa CCM.
Mgombea Urais wa Zanzibar  kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Mwinyi akiwahutubia Wanachama wa CCM wa Wilaya ya Wete Pemba na kuwaomba Kura kumpiga ili kuweza kushinda na kuleta maendeleo kwa Wananchi wa Zanzibar na kuwaombea kura Wabunge,Wawakilishi na Madiwani wa CCM, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Gando Wilaya ya Wete Pemba.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Wete Pemba wakimshangilia Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Mwinyi wakati akiwahutubia na kuwaomba kumpigia kura, mkutano huo umefanyika katika uwanja wa Gando Pemba. 
Mamia wa Wananchi na Wanachama wa CCM wakifuatilia mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe.Dk. Hussein Mwinyi wakati akiwahutubia katika uwanja wa Gando Wilaya ya Wete Pemba. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.