Habari za Punde

Mgombea Urais wa Zanzibar Kwa Tiketi ya CCM Mhe.Dk. Hussein Mwinyi Alipowasiuli Uwanja wa Mkutano wa Kampeni Nungwi Mkoa wa Kaskaziniu Unguja Leo

 

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Mkutano wa Kampeni katika Uwanja wa Mpira wa Nungwi na kuwapungia mkono Wananchi na Wanachama wa CCM wakati akiwasili katika uwanja huo kwa ajili ya kuomba kura kwa Wananchi kuiongoza Zanzibar.

Vijana wa Friends of Mwinyi wakimshangilia Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya CCM Mhe.Dk. Hussein Mwinyi wakati akiwasili katika viwanja vya mpira Nungwi kwa ajili ya mkutano wake wa Kampeni kwa Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.

Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mjumbe wa Halmashari Kuu ya CCM ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, alipowasili katika jukwaa kuu la Viongozi wakati wa hafla wa mkutano wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.

Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Rais Mstaaf wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi, alipowasili katika jukwaa kuu la Viongozi wakati wa hafla wa mkutano wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi alipowasili katika jukwaa kuu la Viongozi wakati wa hafla wa mkutano wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.