Habari za Punde

NHIF ZANZIBAR YAHAMASISHA UMUHIMU WA BIMA YA AFYA NA MAZOEZI

MENEJA  wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Zanzibar Ismail Nuhu Kangeta akizungumza wakati wa Bonanza la michezo kwa watumishi wa Serikali na wananchi Zanzibar lililofanyika kwenye viwanja vya Mau mjini Unguja
MENEJA  wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Zanzibar Ismail Nuhu Kangeta katikati  akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa bonanza hilo
Washiriki wa Bonanza hilo wakiendelea na mazoezi kwenye viwanja hivyo
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwenye bonana hilo

Na.Mwandishi Wetu.                                                                                  
MFUKO  wa Taifa wa Bima ya Afya Zanzibar umehamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa sambamba na ufanyaji wa mazoezi kila wakati kwa ajili ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari na shinikizo la damu.

Hayo  yalisemwa na Meneja Mkaazi wa ofisi ya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Zanzibar Ismail Kangeta wakati akitoa elimu ya umuhimu wa bima ya afya wakati wa bonanza ambalo liliandaliwa na Mfuko huo ofisi ya Zanzibar.

Bonanza  hilo lilikwa na lengo la kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima  ya Afya pia kusisitiza umuhimu wa kushiriki kwenye michezo ili kupunguza magonjwa yasiyoambukizwa ambayo ndio yamekuwa tishio kwa afya za watu kwa sasa.

"Kama  unavyojua ukifanya mazoezi mara kwa mara kuna uwezekano mkubwa wa kuepukana na magonjwa yasiyoyakuambukiza hivyo ndio maana tumeona tuandae bonanza hili na litakuwa linafanyika kila wakati"Alisema.

Hata hivyo aliwataka wananchi kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunifaika na huduma mbalimbali ambazo wamekuwa wakizitoa

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.