Habari za Punde

UZINDUZI WA KAMPENI JIMBO LA PANGANI WAFANA, PANGANI KUTOLEWA PANGOZI NA KUPAISHWA ANGANI

Mgombea ubunge wa jimbo la Muheza Hamisi Mwinjuma (Mwana FA) akimuombea kura kwa wananchi jana mgombea ubunge jimbo la Pangani Jumaa Aweso.
 Sehemu ya wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.
Mgombea ubunge jimbo hilo Jumaa Aweso akiongea na kuomba kura kwa wananchi jimboni humo.
 Sehemu ya wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.
Wagombea ubunge jimbo la Muheza Hamisi Mwinjuma kushoto na Jumaa Aweso wakijadiliana jambo wakati wa uzinduzi huo.
Madiwani wa kata 14 za jimbo hilo wakiwa jukwaani kuomba kura kwa wananchi.

Na Hamida Kamchalla, PANGANI.

Na Hamida Kamchalla, PANGANI.
Mgombea ubunge jimbo la Pangani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso jana aliwataka wananchi wa jimbo hilo kutokubali kufitinishwa na kudanganywa na wapinzani badala yake washikamane na kuichagua ccm ili kuendelea kujiletea maendeleo zaidi.

Aweso alibainisha kwamba atakapochaguliwa kuongoza jimbo hilo kwa miaka mitano tena atamalizia changamoto zote zilizobaki katika utekelezaji wake kwa kipindi kilichopita Jambo litakalobadilisha kabisa taswira ya Pangani na kuupa mji huo hadhi ya utalii.

"Ndungu zangu, wazazi wangu, tuchague viongozi wa ccm kuanzia ngazi ya udiwani hadi raisi wetu ili tumalizie pale palipobaki katika utekelezaji, msikubali kuyumbishwa wala kufitinishwa na wapinzani, nataka niitie Pangani pangoni niipaishe angani na kuipa hadhi ya utalii" alisema Aweso.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.