Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi wakisikiliza sera za mgombea uwakilishi kwa jimbo la kwahani Yahya Abdalla Rashid (hayupo pichani ) huko katika Uwanja wa Jimbo la Kwahani Zanzibar .
Picha na Khadija Khamis - Maelezo Zanzibar.
Na.Sabaha Khamis - Maelezo Zanzibar.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi kukipigia kura Chama hicho ili kuendelea kuwaletea maendeleo nchini.
Amesema hayo wakati wa kuwatambulisha wagombea wa Ubunge, Uwakilishi na Udiwani wa Jimbo la Kwahani katika uzinduzi wa Kampeni iliyofanyika uwanja wa branch ya Kwahani.
Amesema wananchi wasipoteze kura zao kwa kuwapigia wagombea wasiowakweli na badala yake wawachaguwe wagombea wa Chama Cha Mapinduzi ambao sera zao ni zakuleta maendeleo.
Ameeleza kuwa Jimbo la Kwahani ni Jimbo lakupigiwa mfano kwani ni Jimbo lilitoa Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Chama cha Mapinduzi.
Hata hivyo amewaomba kuwapigia kura Mgombea wa Urais wa Jamuhuri ya Muungani wa Tanzania Dk. John Joseph Magufuli, Mgombea Mwenza Mama Samia Suluhu Hassan, Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi pamoja na Wabunge,,Wawakilishi na Madiwani kupitia chama hicho .
Nae Mgombea Ubunge Jimbo hilo Ahmed Yahya Abdul-wakil amewataka wanachama wa Jimbo la Kwahani kumpigia kura na kumpa ushindi wa kishindo kwani kufanya hivyo nikukipa nguvu chama hicho ili kiendelee kushika dola .
Ameahidi kuvaa viatu vya Dk. Mwinyi ili kuleta maendeleo katika Jimbo hilo, kuimarisha vikundi vya Wajasiriamali kwa kuwapatia mitaji, kuwatafutia kituo cha kisasa kuweza kuuza bidhaa zao,kuwaendeleza wasanii na michezo ndani na nje ya nchi.
Pia Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Kwahani amesema iwapo atapewa ridhaa ya kuongoza katika Jimbo atashirikiana na Wagombea wenzake kuimarisha maendeleo ya Jimbo hilo.
Pamoja na hayo baadhi ya Wagombea ambao kura zao hazikutosha wameahidi kushirikiana na walioteuliwa ili kuhakikisha wanakipatia ushindi chama hicho katika uchaguzi mkuu 28 Okt 2020.
No comments:
Post a Comment