Habari za Punde

Waandishi wa Habari Pemba Wapata Mafunzo ya Mabadiliko ya Sheria ya Kodi ya Mapato Zanzibar.

Meneja Uhusiano na Huduma kwa walipakodi kutoka ZRB Shaaban Yahya Ramadhani, akitoa maelezo juu ya mabadiliko mbali mbali ya sheria za kodi za bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), kwa waandishi wa habari Kisiwani Pemba, mkutano uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Gombani
Meneja Uhusiano na Huduma kwa walipakodi kutoka ZRB Shaaban Yahya Ramadhani, akielezea kwa mifano hai juu ya mabadiliko ya sheria pamoja na wafanyabiashara kuifahamu namba ya utambulisho (control Number) itakayowawezesha wafanyabiashara hao kulipa kodi kwa urahisi, mkutano uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Gombani
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbali mbali vya habari Kisiwani Pemba, wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa mabadiliko ya sheria za kodi za Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), mkutano uliofanyika katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Gombani
Mwandhishi wa Habari kutoka Redio Jamii Micheweni Ali Massoud Kombo (aliyefunga mikono), akimsikiliza kwa makini meneja Uhusiano na Huduma kwa walipakodi kutoka ZRB Shaaban Yahya Ramadhani, akijibu swali lake juu ya mashuala ya mabadiliko ya sheria za Bodi ya Mapato Zanzibar, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Gombani.

Meneja wa Huduma Nyenginezo kutoka Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Ofisi ya Pemba Abeid Omar Salim, akielezea kwa vitendo umuhimu kwa wafanyabiashara kuifahamu namba ya utambulisho (control Number), wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Gombani.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.