Habari za Punde

Wakandarasi wa Mradi wa Ujenzi Jengo la Mahkama Kuu Zanzibar Watakiwa Kuharakisha Ujenzi Huo.

Muonekano wa jengo jipya la mahakama ya Zanzibar inayoendelea kujengwa huko Tunguu wilaya ya kati Mkoa wa kusini Unguja .
Waziri wa fedha na mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa akielekeza jambo kwa wahandisi na wakandarasi wakati alipofika kuangali jengo la Mahakama linaloendelea kujengwa huko Tunguu Wilaya ya Kati Unguja.
Waziri wa fedha na mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa akisikiliza maelekezo kutoka kwa mkandarasi wa jengo la mahakama mpya ya Zanzibar Navaneeth Anbazhagan.wakati alipofika kuangali jengo hilo linaloendelea kujengwa Tunguu Wiaya ya Kati Unguja.
Waziri wa fedha na mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa akilitembelea Jengo la Mahkama  linaloendelea kujengwa huko Tunguu Wilaya ya Kati Unguja .
PICHA NA FAUZIA MUSSA/ MAELEZO

Na.Fauzia Mussa - Maelezo  Zanzibar.  07/09/2020
Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa amewataka wakandarasi wanaojenga Mahakama kuu ya Zanzibar kuharakisha ujenzi huo ili ukamilike kwa wakati.
Alisema hayo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo na ubora wa ujenzi wa Mahakama hiyo unaondelea katika kijiji cha Tunguu Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Balozi Ramia amesema kuwa jengo hilo lilitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Octoba kwa lengo la kuanza kazi lakini kwa hatua iliofikia hivi sasa ni vigumu kukamilika wakati huo.
Alisema kuwa Serikali inatoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi, hivyo amewataka wakandarasi wawe makini na kuzingatia muda waliokubaliana ili kuepusha changamoto na hasara za kifedha.
 “Majengo ya Mahakama hayajengwi mara kwa mara hivyo ubora unahitajika na muda tuliokubaliana,ikiwa pesa zinatolewa kwa nini jengo linazorota” alisema Waziri.
Akielezea kuchelewa kwa ujenzi huo, Mhandisi wa jengo la Mahakama hiyo Mussa Ali Hamad alisema kukosekana kwa baadhi ya vifaa kulikosababishwa na mripuko wa maradhi ya Corona na kutopatikana kwa rasilimali ya mchanga kwa wakati ndio sababu zilizopelekea kuzorota ujenzi huo.
Pia Mhandisi huyo ameiomba Serikali kuwaongezea wafanyakazi ili waweze kufanyakazi masaa 24 na hatimae kukamilisha kazi hiyo kwa haraka

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.