Habari za Punde

Wananchi wa Jimbo la Donge Wametakiwa Kutofanya Mzaha na Dharau.

 Na Ali Issa Maelezo Zanzibar 23/92020

Wananchi wa Jimbo la Donge wametakiwa kutofanya mzaha na kudharau kwenda kupiga kura kuwachagua viongozi Chama Cha Mapinduzi ili kiendelee kuongoza katika ngazi ngazi zote za Taifa.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi  Mkoa wa Kaskazini Iddi Ali Ameir wakati wa uzinduzi wa kampeni za Jimbo hilo na kuwanadi wagombea  nafasi ya Ubunge, Uwakilishi na udiwani zilizofanyika katika Uwanjavya Misuka Mahonda Wilaya ya Kaskazini B Unguja.

Amesema Jimbo la Donge liko imara katika kutekeleza na kusimamia chama na limejipanga kuwashajihisha wananchi kutumia fursa ya kuwachagua viongozi CCM katika nafasi zote.

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura  ili chama kiweze kushinda kwa kishindo na kuendelea kushika Dola kwa kupeperusha bendera hiyo.

“Ili kufanikisha dhamira ya kupata ushindi nataka mjitokeze kwa wingi bila ya kufanya mzaha au kupuza”, alisema Iddi Ali.

Aidha aliwasisistiza kuwa wasijaribu kuchagua viongozi wanaohubiri siasa za uchochezi na ubaguzi wakiwa na nia ya kuleta machafuko na uvunjifu wa amani iliopo nchini.

Nae Mgombea wa nafasi ya Uwakilishi Jimbo hilo Khalid Mohamed Salum alisema katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi jimbo la Donge limefanikiwa kutimiza ahadi zake kwa asilimia 96 kwa kueneza maji, umeme na kuchimba visima 12 katika maeneo mbalimbali ya Jimbo hilo.  

Mgombea huyo alieleza kuwa walifanikiwa kujenga barabara za ndani kwa viwango vya kifusi na lami, kutoa pembejeo kwa wakulima maeneo mbali mbali bila kuzingatia chama, kuwawekea mazingira mazuri ya Elimu na afya.

Dkt Khalidi alifahamisha kuwa mafanikio hayo yote yanatokana na ushirikiano uliopo ndani ya jimbo na Serikali ya mkoa chini ya uongozi makini wa awamu ya saba.

Nae mgombea wa nafasi ya ubunge Sud Mohamed Juma alisema kua akipata ridhaa ya kuchaguliwa wanachi wajimbo hilo wajiandae kuimarisha kilimo cha kijani ambacho kinatija kubwa kwakulima

Alisema atajikita hapo zaidi kwani vile yeye ni mtaalam wa masuala ya hayo.

Aliahidi kumalizia yale yalio fanywa na walio mtangulia na kusema kua anahitaji ushirikiano kufanikisha hayo.    

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.