Habari za Punde

Wajasiriamali Kisiwani Pemba Wamtaka Mgombea Urais wa Zanzibar Kwa Tiketi ya CCM Dk. Hussein Mwinyi Kutafuta Ufumbuzi wa Mlundikano wa Kodi.

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi, akizungumza na Wafanyabiashara na wajasiriamali wa kisiwa cha Pemba, katika ukumbi wa kiwanda cha makonyo cha Shirika la Biashara Zanzibar (ZSTC).
BAADHI ya Wafanyabishara na wajasiriamali wa kisiwa cha pemba wakimsikiliza Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi uko katika kiwanda cha makonyo Pemba.

Na.Is-Haka Omar - Pemba.

WAFANYABIASHARA na wajasiriamali Kisiwani Pemba wameiomba serikali ijayo ya awamu ya nane kutafuta ufumbuzi wa mlundikano wa kodi.

Rai hiyo wameitoa katika mwendelezo wa ziara ya mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi, huko katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Fidel Castro Pemba.

Walisema kodi wanazolipa zimekuwa ni nyingi kuliko mitaji yao hali inayochangia wafanyabishara wengi kisiwani Pemba kutopata maendeleo waliyakusudia.

Walimuomba mgombea huyo wa kiti cha urais kwa tioketi ya CCM Dk.Hussein, endapo atakuwa rais ahakikishe anaweka mfumo rafiki wa utoaji wa kodi kwa wafanyabiashara hao.

Pamoja na hayo wafanyabishara hao walisema bado kuna changamoto ya huduma za usafiri kwani boti na ndege za kusafirisha mizigo ni kidogo.

Aidha,walieleza kwamba bado kuna changamoto ya ukodsefu wa bandari kubwa za kisasa zenye uwezo wa kutoa huduma nyingi kwa wakati mmoja.

Sambamba na hayo wafanyabiasha hao walimuomba mgombea huyo aimarishe ujenzi wa miundombinu ya barabara za ndani na kubwa na za (Flyover), kwa lengo la kurahisha shughuli za kibiashara.

Akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja za wafanyabiashara hao mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi, alisema lengo lake ni kufanya mapinduzi ya kibiashara nchini.

Alisema lengo la kuzungumza na wafanyabishara hao ni kuzijua mapema changamoto zinazowakabili ili akiingia madarakani aanze kazi ya kuzitatua.

Dk. Mwinyi, aliahidi kuwa akiingia madarakani atahakikisha anafanya mageuzi makubwa kwa kutizama upya mfumo wa kodi ili uwe rafiki kwa wafanyabiashara hao.

Alisema kodi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi hivyo serikali haiwezi kuiondosha badala yake itaweka utaratibu mzuri ambao hautowaumiza wafanyabiashara.

Pamoja na hayo aliahidi kuimarisha mbiundombinu ya usafirishaji ili kurahisisha gharama za usafirishaji.

Alisema atajenga bandari kubwa kwa upande wa Unguja na Pemba kwa lengo la kwenda sambamba na falsafa ya maendeleo endelevu kupitia uchumi wa bahari (Blue Economy).

Aliyashauri mabaraza ya manispaa na halmashauri za Wilaya kubuni mikakati ya kujenga masoko makubwa na vituo vya magari vya kisasa ili kutengeneza mazingira mazingira mazuri ya kibiashara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.