Habari za Punde

SOS Yakabidhi Hundi ya Shs.Milioni Arubaini Halmashauri ya Micheweni Pemba.

MJUMBE wa Bodi ya Shirika lisilo la kiserikali Zanzibar SOS Dk Issa Seif Salim, (kushoto) akimkabidhi hundi ya shilingi Milioni 40,156,000/= kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni Ndg.Hamad Mbwana Shehe, kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa kituo cha afya ya mama na Mtoto shehia ya Tumbe Wilaya ya Micheweni, fedha hizo zimetolewa na SOS kupitia mradi wa kuimarisha Familia.
AFISA Mdhamini Wizara ya Habari Vijana na Utamaduni Pemba Fatma Hamad Rajab, akimkabidhi Mkuu a Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadid Rashid, boti ya kuvulia pamoja na vifaa vyake ikiwemo Nyavu 10, mashine na maboya kwa ajili ya vijana wa Baraza la Vijana Misooni Wilaya hiyo, ikiwa ni utekelezaji wa Programa ya ajira kwa vijana ya Bilioni 7 iliyoanzishwa Rais Mstaafu wa awamu ya Saba wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.