Habari za Punde

TAKWIMU ZAIPAISHA TANZANIA UCHUMI WA KATI -SERIKALI

 A

A     Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Anjelina Lutambi (aliyesimama) akitoa ufafanuzi kwenye mkutano wa uelimishajiwa zoezi la ukusanyaji wa takwimu za mifugo,kilimo na uvuvi katika Kijiji cha  Msikii, Kata ya Muhamo, Mkoani Singida hivi karibuniB

A.      Bibi Salma Mkumbo akiuliza swali kwa wataalamu kwenye mkutano wa uelimishaji wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu za mifugo,kilimo na uvuvi katika Kijiji cha  Msikii, Kata yaMuhamo, Mkoani Singida hivi karibuni c

A.      Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa (aliyesimama) akitoa ufafanuzi kwenye mkutano wa uelimishaji wa zoezi la ukusanyaji wa takwimu za mifugo,kilimo na uvuvi katika Kijiji cha  Msikii, Kata yaMuhamo, Mkoani Singida hivi karibuniDMeneja Takwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mkoa wa Singida, Naing’oya Kipuyo( aliyesimama) akitoa maelezo kwa  katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Anjelina Lutambi (mwenye miwani) na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) kwenye ofisi ya Serikali ya kijiji cha Msikii, Kata yaMuhamo, MkoaniSingidaHivikaribuniE

Elibariki Musa, Mkazi wa kijiji cha Msikii, Kata yaMuhamo, MkoaniSingida akiuliza swali kwa wataalamu (Pichana John Mapepele). 

Na John Mapepele, Singida 

Serikali imesema takwimu sahihi zilizokusanywa kutoka kwenye sekta mbalimbali za kimkakati za Mifugo, Kilimo na Uvuvi nchini zimeifanya Tanzania chini ya Uongozi wa Rais wa Awamu ya Tano Mheshimiwa John Pombe Magufuli kuingia kwenye Nchi za Uchumi wa Kati duniani.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na ujumbe maalum wa kitaifa ulioongozwa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Anjelina Lutambi wakati  walipokuwa wanakagua zoezi la kitaifa ya ukusanyaji taarifa za kina za Kilimo, Mifugo, ufugaji wa samaki Mkoani Singida ambalo  limekamilika  hivi karibuni kwa mafanikio makubwa.

“Madhumuni makuu ya Sensa hii ni kupata taarifa muhimu za kilimo, mifugo na uvuvi zitakazotumika katika kupanga na kutathmini utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya sekta katika taifa la Tanzania, na endapo ukusanywaji wa takwimu utakuwa kwenye ubora unaositahili utasaidia kulifanya taifa kupea kwenye uchumi wa juu kabisa katika kipindi kifupi kijacho” ameongeza Dkt. Chuwa

Akifafanua amesema taarifa  kwa mfano za magonjwa ya mifugo na mazao zitaisaidia Serikali kuainisha maeneo yanayokabiliwa na visumbufu/magonjwa  ili kuchukua hatua stahiki na kupanga mipango ya kudhibiti.Pia taarifa kuhusu uzalishaji wa mazao zitasaidia kujua kiasi cha uzalishaji kwa maeneo husika na kuiwezesha Serikali kupanga upatikanaji wa masoko na uwezekano wa kuanzisha viwanda vya kusindika mazao hayo.

Aidha amesema taarifa kuhusu upatikanaji na matumizi ya ardhi zitatumika kupanga mipango ya matumizi bora ya ardhi vijijini  hivyo zitatumika kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji hapa nchini.

Dkt. Chuwa ameongeza kuwa matokeo ya Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yanatarajiwa kuweka msingi imara wa sekta hii kwa miaka mingi iyajo, kwa  kuwa Sekta ya Kilimo ina umuhimu mkubwa  kwenye mustakabali wa maisha ya binadamu kwa kuwa ndiyo chanzo cha chakula na malighafi zinazohitajika katika viwanda hususani katika awamu hii inayoongozwa na dira ya uchumi wa viwanda.

“Kutokana na umuhimu huo, na kupitia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia ya Mwaka 2030, Sekta ya Kilimo ilipewa Lengo la Pili  la Kutokomeza Njaa, Kuwa na Uhakika wa Chakula, Lishe Bora na Kukuza Kilimo Endelevu. Aidha, lengo hilo limesisitiza umuhimu wa kuongeza tija katika sekta ya kilimo kwa kuongeza thamani ya mazao na pia kusisitiza matumizi bora ya ardhi na kurutubisha udongo, ili kuongeza uwezo wa binadamu kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya tabianchi na athari zake yakiwemo majanga mbalimbali kama mafuriko na ukame pamoja na majanga mengine ikiwemo ndege waharibifu” ameeleza Dkt. Chuwa

Dkt. Lutambi amesisitiza kuwa pamoja na faida za jumla ambazo mkulima atakazozipata Sensa hii itamsaidia mtu mmoja mmoja kutatua changamoto mbalimbali katika kilimo,mifugo na uvuvi hasa upatikanaji wa pembejeo, huduma za ugani, upatikanaji wa masoko kwa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Ameongeza kuwa takwimu ni kitu cha msingi katika kupanga maendeleo kuanzia kwenye ngazi ya kijiji hadi taifa kwa kuwa zinasaidia kuonyesha changamoto na mafanikio na hivyo kusaidia kupata ufumbuzi wa kudumu wa changamoto hizo.

“Ni muhimu tukafahamu kuwa takwimu sahihi za mifugo, mazao na uvuvi zitasaidia  uchangiaji wa malighafi za  viwanda  vyetu hivyo kukuza uchumi wetu ambao tunautaka wa viwanda” amesisitiza Dkt. Lutambi

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Mohamed Bashe, kwenye hotuba yake, wakati  wa ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi wa Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Kilimo 2019/20, iliyofanyika katika Ukumbi wa TMDA,Mwanza Julai, 25 mwaka huu alisisitiza Mwaka huu 2020, Benki ya Dunia imeitangaza Tanzania kuwa katika kundi la nchi zenye uchumi wa kipato cha kati, ambapo alisema Taarifa hizi zimeleta faraja kubwa kwa sekta ya kilimo  kwa kuwa ndiyo iliyotoa mchango mkubwa zaidi katika Pato la Taifa wa asilimia 26.6 mwaka 2019 na pia inatoa ajira kwa takribani asilimia 66 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi.

“Sekta ya kilimo ilichangia asilimia 24.3 ya mapato ya mauzo nje ya nchi mwaka 2019. Fedha hizi kwa kiasi kikubwa zinatumika nchini katika mambo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu wezeshi ya barabara, reli, maji, usambazaji umeme na kuimarisha miundombinu ya kutolea huduma za jamii kama vile afya na Elimu kwa lengo la kuimarisha maendeleo ya wananchi” alifafanua Dkt. Bashe

Aliongeza kuwa, kwa mujibu wa Ripoti ya Tathmini ya Umasikini Tanzania Bara ya Mwaka 2018, sekta hii ikiendelezwa vyema ndio pekee yenye uwezo wa kuleta maendeleo jumuishi nchini, hivyo  kuna umuhimu mkubwa wa zoezi la sensa ya mifugo, mazao na uvuvi likafanyika kwa ubora na kwa umakini  unaositahili.

Pia wakati wa tukio la uzinduzi wa mafunzo ya wadadisi wa Sensa hii, Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Amina Msengwa amesisitiza kuwa takwimu zina mchango mkubwa katika maandalizi na utekelezaji wa sera na mipango, na vile vile katika kufanya maamuzi sahihi yanayotakiwa kufikiwa kwa kutumia ushahidi stahiki (evidence based decision making).

 Amesema Sensa ya Mwaka wa Kilimo 2019/20, ni ya tano kufanyika hapa nchini tangu nchi ipate uhuru na inafanyika kwenye jumla ya maeneo yaliyochaguliwa ya kuhesabia 2,820 ambapo kutokana na maeneo hayo kaya 33,807 kutoka Tanzania bara na Zanzibar.

Kwa upande wake, Meneja Takwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mkoa wa Singida, Naing’oya Kipuyo ameishukuru Serikali ya Mkoa wa Singida kwa kusaidia kufanikisha zoezi hili ambalo  limefanyika kwa takribani siku 50 ambapo pia amewapongeza wananchi kwa kutoa ushirikiano wa  kutosha.

Kipuyo amesema taarifa zilizokusanywa kwenye Sensa hii ni za kipindi cha kuanzia tarehe 1 Oktoba, 2019 hadi tarehe 30 Septemba, 2020 na kuongeza kuwa Mkoa wa Singida umekamilisha zoezi hilo kwa maeneo yote ambapo maeneo madogo ya kuhesabia watu yaani Enumaration Areas (EA) 90 yenye kaya 1087 zilizochaguliwa kwa ajili ya kufanyiwa sensa hii zilifikiwa

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.