Habari za Punde

Benki ya Taifa ya Biashara NBC kutoa ushirikiano na Wizara ya Afya Zanzibar

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii Jinsia na Watoto Halima Maulid Salum akizungumza na uongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo Theobald Sabi Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Theobald Sabi akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii Jinsia na Watoto Halima Maulid (hayupo pichani) juu ya dhamira yao ya kutaka kusaidia katika sekra ya Afya walipofika Ofisini kwake Mnazimmoja. Kulia ni Msemaji wa Benki hiyo William Kalloge.

 

Picha na Makame Mshenga


Na Fatma Kassim

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii Jinsia na Watoto Halima Maulid Salum ameuhakikishia uongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC)kuwa Wizara ya Afyaa iko tayari kushirikiana na beki hiyo katika kutoa huduma za afya kwa wananchi wa Zanzibar ili kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane.

Naibu Katibu Mkuu huyo aliyasema hayo leo huko Ofisini kwake Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Uongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo Theobald Sabi akiwa amefuatana na Meneja Uhusiano William Kallaghe na Ramadhan Lesso ambaye ni Meneja wa Tawi la NBC Zanzibar.

Amesema hatua ya Benki ya NBC ya kushirikiana na Wizara ya Afya ni jambo kubwa ambalo litalinufaisha taifa kwa kuwapatia huduma bora wananchi wake wa Unguja na Pemba hasa kwa mama na watoto.

Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara Theobald Sabi alimueleza Naibu Katibu Mkuu huyo azma ya Benki yake ya kusaidia gari ya kuchukulia wagonjwa ambayo itajikita zaidi kwa upande wa akina mama na watoto.

Alimueleza Naibu Katibu Mkuu huyo kwamba Benki yake iko tayari na gari hiyo itawasilishwa wiki ijayo hapa Zanzibar kwa azma ya kuikabidhi na kuendelea na shughuli hizo za kutoa huduma za afya kwa akina mama na watoto.

Mkurugenzi huyo pia aliomba uongozi wa Wizara ya Afya kuwapa maeneo ama aina ya misaada ikiwemo vifaa na dawa vinavyohitajika pamoja na gharama zake ili waweze kusaidia

Aidha, Mkurugenzi huyo alimueleza Naibu Katibu Mkuu huyo azma yao ya kusaidia dawa pamoja na vifaa kwa ajili ya hospitali mbali mbali ambazo wataelekezwa.

Pia, Mkurugenzi huyo alimueleza Naibu Katibu Mkuu huyo shughuli zinazofanywa na Benki hiyo ikiwa ni pamoja na aina za misaada inayotolewa ikiwemo ile ya elimu, nafasi za masomo, afya, kuwasaidia wajasiriamali wakiwemo vijana.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.