Habari za Punde

Maendeleo ya ujenzi wa Soko la muda la Kibanda Maiti

Maendeleo ya ujenzi wa Soko la muda la Kibanda Maiti ukiendelea ikiwa ni kutekeleza ahadi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dr Hussein Ali Mwinyi alipozungumza na wafanyabiashara siku kadhaa baada ya kuteuliwa kuwa Rais katika soko la Kijangwani

Mafundi wakiendelea na ujenzi katika soko la muda la Kibanda maiti. Ikumbukwe kwamba wafanyabiashara walihamishwa soko la Marikiti Darajani kipindi cha cha mripuko wa maradhi ya Corona na kuhamishiwa Kijangwani kwa muda ambapo eneo lile lilikuwa kwa ajili ya kutengenezwa kituo kikuu cha Daladala na walipotaka kuhamishwa kupelekwa Daraja Bovu waligoma kwa kuwa si sehemu ya biashara na Rais kuingilia kati suala hili na kuahidi kulitafutia ufumbuzi.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.