Habari za Punde

Mbunge wa Jimbo la Fuoni Zanzibar Mhe Abass Mwinyi Aipongeza Skuli ya Juba Islamic Kwa Kuweka Kipaumbele Somo la Sayansi.

Na,Takdir Suweid Zanzibar.

Mbunge wa Jimbo la Fuoni Kepten Abasi Ali Mwinyi ameupongeza uongozi wa Skuli ya Juba Islamic kwa kuweka kipao mbele masomo ya Sayansi ili kuweza kufikia azma ya Serikali ya awamu ya nane ya kufikia Uchumi wa Buluu.

Amesema hatua hiyo itapelekea Zanzibar kupata Wataamu Wazalendo wa fani mbalimbali watakoweza kuitumikia nchi yao na kuleta maendeleo.

Akizungumza kwa niaba yake Diwani wa kuteuliwa Wilaya ya Magharibi B Thuwaiba Jeni Pandu katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo wakati wa Mahafali ya Sita ya Skuli ya Juba Islamic iliopo Fuoni Jitimai Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Wadau wa elimu ili kuhakikisha Wanaleta mabadiliko ya kielimu, yatakayowawezesha Wananchi kujiajiri kupitia Ujasiriamali na kuepuka kutegemea Ajira Serikali pekee.

Amesema bila ya Wataalamu Wazalendo malengo ya Serikali hayatoweza kufikiwa hivyo ni vyema kwa Skuli nyengine kuiga mfano huo kwa kuyapa kipao mbele masomo ya Sayansi.

Mapema Msaidizi Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo amesema wamefanikiwa kusaidia Serikali kuondosha Ujinga,Watoto wa Mitaani na kushajiisha Wanafunzi wa kike kusoma masomo ya Sayansi ili kuweza kupata wataamu ikiwemo Madaktari na Wahandisi.

Wakati huo huo Makamo Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Maandalizi na Msingi Mambosasa Othaman Yussuf Suleiman amewakumbusha Wazazi na Walezi kufuatilia maendeleo ya Watoto wao ili kubaini changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi.

Akizngumza katika mahafali ya kwanza ya Skuli hiyo amewataka Wazazi na Walezi kuwashajiisha Watoto wao kuacha kutumia muda mingi kuangalia michezo ya Tv na badala yake wazidishe bidii kudurusu masomo yao ili waweze kufaulu vizuri Mitihani yao ya Taifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.