RAIS wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali
inahitaji sana kuwepo shughuli za Uwekezaji ili kuharakisha kasi ya maendeleo
na kukuza uchumi wa Taifa.
Dk. Mwinyi amesema hayo Ikulu Jijini Zanzibar alipokutana ujumbe wa Wawekezaji wa Kampuni ya Ozuaydin kutoka nchini Uturuki, ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu Mahmet Aydin ambao umeonyesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa Bandari, uwekaji wa vifaa pamoja na uendeshaji wa shughuli za Bandari eneo la Malindi na Mpigaduri, sambamba na ujenzi wa Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano.
Alisema Serikali iko tayari kushirikiana na Wawekezaji kwa kuhakikisha inaweka mazingira mazuri yanayovutia ili kufanikisha azma hiyo.
Aliwataka wawekezaji hao kuwasiliana na mamlaka zinazosimamia Uwekezaji nchini, ili kupata miongozo na taratibu za kisheria zinazohusiana na jambo hilo.
Nae, Mkurugenzi Mkuu kutoka Kampuni ya Uzuaydin, Mahmet Aydin alisema Kampuni yake imedhamiria kutumia fursa za uwekezaji zilizopo nchini baada ya kuridhishwa na mazingira bora yaliopo.
Alisema amefurahishwa na mapokezi mazuri ya Serikali aliyoyapata na kubainisha uwekezaji wanaolenga kuufanya utakuwa na tija na maslahi kwa wananchi wa Zanzibar pamoja na nchi za ukanda huu.
Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024
2231822
E-mail: abdya062@gmail.com
No comments:
Post a Comment