Na Maulid Yussuf WEMA
Taasisi ya Elimu ya Zanzibar inaendelea kupitia vyema mtaala wa elimu ya maandalizi na msingi ili Taifa lipate Elimu bora.
Hayo yameelezwa na Meneja wa mtaala na vifaa kutoka Taasisi ya elimu ya Zanzibar mwalimu Abdallah Mohamed Mussa, wakati akifungua kikao cha siku moja kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo katika ukumbi wa ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mazizini mjini Unguja.
Amesema upitiaji wa Mtaala ni Safari ndefu kwani ilianza tokea January 2019 kwa kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbali mbali kwa ajili ya kutoa maoni yao ili kupata mtaala ulio bora katika nchi.
Amesema katika kufanikisha hilo Taasisi imefanikiwa kupitia mitaala ya nchi 12 ili kulingalisha na kupata uzoefu katika masuala ambayo mtaala wa Zanzibar hayamo kwa lengo la kuimarisha na kupata mtaala bora kwa wanafunzi.
Amefahamisha kuwa katika mtaala huo mpya baada ya kukamilika wana mategemeo makubwa kuwa watoto watakaomaliza Elimu ya maandalizi wataweza kujua kusoma, kuandika na kuhesabu pamoja na kuwa na ubunifu kwa mujibu wa daraja lake la elimu ambao utaweza kumjenga kadri anavyokuwa na kuweza kujiajiri hapo baadae.
Amesema kikao hicho ni kina lengo la kupitia mawanda na mtiririko mtaala ya Skuli za maandalizi, hivyo amewataka kuitumia nafasi hiyo na kushauri kutoa maoni kwa kuwaangalia zaidi watoto wetu ili kupata elimu bora nchini.
Nae msaidizi wa kituo cha Taifa cha Walimu NTRC mwalimu Mohammed Khamis Suleiman amesema upitiaji wa mtaala ni jambo muhimu sana na Taasisi ya Elimu imeamua kuweka makundi mbalimbali kwa lengo la kutoa maoni yao juu ya mawanda hayo ili kuweza kufikia malengo ya nchi.
No comments:
Post a Comment