Habari za Punde

Taasisi za waangalizi wa ndani wa uchaguzi mkuu 2020 wakabidhi ripoti kwa Tume ya Uchaguzi


Mwenyekiti wa Taasisi wa  waangalizi wa ndani wa Uchaguzi Mkuu 2020 Abdalla Maulid Diwani akisoma muhutasari wa taarifa ya waangalizi  na kumkaribisha mgeni rasmi katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Dok.Ali Mohamed Shein katika Ofisi za ZURA.
Mwenyekiti wa Taasisi wa  waangalizi wa ndani wa Uchaguzi Mkuu 2020 Abdalla Maulid Diwani akisoma muhutasari wa taarifa ya waangalizi  na kumkaribisha mgeni rasmi katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein katika Ofisi za ZURA.

Makamo Mwenyekiti Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mabrouk Jabu Makame akizungumza na waangalizi wa Uchaguzi wa ndani na viongozi wa vyama vya siasa wakati wa  kupkea taarifa ya uchaguzi uliofanyika Oktoba mwaka huu katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein, Ofisi za ZURA.
Makamo Mwenyekiti Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mabrouk Jabu Makame akionyesha  kitabu cha taarifa ya wangalizi wa ndani wa Uchaguzi Mkuu Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya waangalizi wa ndani Abdalla Diwani katika Ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein, Ofisi za ZURA .
Mwenyekiti wa Taasisi ya  waangalizi wa ndani wa Uchaguzi Mkuu 2020 Abdalla Diwani akionesha cheti maalum alichokabidhiwa na Makamo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mabrouk Jabu Makame katika hafla ilyofanyika Ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein, Ofisi za ZURA

Makamo Mwenyekiti Tume ya Uchaguzi Zanzibar  Mabrouk Jabu akisisitiza jambo katika hafla ya kupokea taarifa ya wangalizi wa ndani wa Uchaguzi wa 2020 katika Ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein, Ofisi za ZURA.

PICHA NA FAUZIA MUSSA /MAELEZO ZANZIBAR.


Na Sabiha Khamis   Maelezo      23/12/2020

Makamo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mabrouk Jabu Makame amesema asasi za kiraia ni wadau wakubwa katika suala la demokrasia ambao wanaweza kupeleka mbele maendeleo kwa kasi kubwa ikiwa watasimamia vyema nafasi zao.

Amesema waangalizi wa uchaguzi ni watu muhimu sana katika kufanikisha maendeleo ya uchaguzi wa Demokrasia ukizingatia kwamba taarifa za makundi ya waangalizi husaidia Tume ya uchaguzi kufanya marekebisho ya sheria za uchaguzi ili kuboresha chaguzi zinazofuata.

Makamo Mwenyekiti wa ZEC ametoa maelezo hayo alipokuwa akizungumza na waangalizi wa ndani wa uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika mwezi Oktoba na viongozi wa vyama vya siasa baada ya kupokea taarifa kutoka kwa waangalizi hao katika Ukumbi wa Dk. Ali Mohamed Shein uliopo Ofisi za ZURA Maisara.

Amewataka viongozi wa Taasisi za wangalizi wa uchaguzi wa ndani kuendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwa jamii ili iweze kushiriki kikamilifu katika masuala ya kidemocrasia.

Aliwaeleza waangalizi wa uchaguzi wa ndani kwamba wapo wananchi wamepoteza vitambulisho vya kupigia kura na wanaotaka kuhama kutoka eneo moja la uchaguzi kwenda jengine waliotimiza vigezo vya sheria hivyo wanahitaji kuelimishwa ili kupata haki yao hiyo ya msingi

kuwa huduma hizo zinapatikana katika ofisi za Wilaya kwa siku za kazi na muda wa kazi” alisema Makamo Mwenyekiti.

Amewapongeza viongozi wa Taasisi hiyo kwa kazi nzuri waliofanya katika kipindi chote cha zoezi la uchaguzi mkuu  wa 2020 na kuandaa taarifa ambayo imegusa maeneo yote ya Zanzibar.

Ameahidi kuifanyia kazi taarifa ya waangalizi wa uchaguzi wa ndani na kuyifanyiakazi mapendezo yaliyowasilishwa ili kufanya chaguzi bora za kitaifa, kikanda na Kimataifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Uangalizi wa Ndani wa Uchaguzi Abdalla Maulid Diwani ameishukuru Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa kuwapatia kibali cha uangalizi wa uchaguzi wa mwaka 2020.

Alishukuru kwa kupatiwa mafunzo ya sheria za uangalizi wa uchaguzi yaliyowasaidia kukamilisha zoezi hilo kwa umahiri na umakini wa hali ya juu.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.