Habari za Punde

TIRA na Mashirika ya Bima Zanzibar yampongeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango

Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt. Mussa Juma akitoa maelezo juu mashirikiano waliyonayo na makampuni ya Bima yanayotoa huduma zake Zanzibar katika hafla ya kumpongeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali iliyofanyika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Bima Zanzibar Abdulnasir Ahmed Abdulrahman akitoa pongezi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali kwa kuteuliwa na Rais kuiyongoza Wizara hiyo.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Khamis Mussa akichangia kitu katika hafla ya kumpongeza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali hafla iliyofanyika Wizarani Vuga.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali akizungumza na watendaji wakuu wa Makampuni ya Bima yanayotoa huduma zake Zanzibar yakiongozwa na Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali akizungumza na watendaji wakuu wa Makampuni ya Bima yanayotoa huduma zake Zanzibar yakiongozwa na Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali (katikati) katika picha ya pamoja na Wiongozi wa Bima Zanzibar na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).

Picha na Makame Mshenga.


Waziri wa  nchi ofisi ya Raisi Fedha na Mipango Zanzibar Jamali Kassim Ali amewataka Watendaji wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) na Makampuni ya Bima kuipitia Mifumo ya Utoaji wa Fidia kwa Wateja wao ili kuweza kuongeza Wateja, kuondoa usumbufu na kuiingizaia Serikali Mapato.

 

Amesema baadhi ya Mifumo ya Bima inawakwaza Wateja wakati wanapopata ajali na kupelekea kukata tama hivyo iwapo wataipitia Mifumo hiyo na kifanyia marekebisho,itaweza kuisaidia jamii, kuwa kivutio kwa Wateja na kuongeza idadi na kuisaidia Serikali kupata Maendeleo.

 

Akizungumza na Viongozi wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA) na Makampuni ya Bima waliofika ofisini kwake kubadilishana mawazo ili kuweza kufikia malengo ya Uchumi wa Buluu amesema Serikali itaendelea kutoa msukumo ili malengo ya kupata maendeleo yaweze kufikiwa.

 

Amesema Sekta ya Bima inaweza kutoa mchango mkubwa katika kuiingizia Serikali Mapato lakini bado mwamko wa Wananchi juu ya kukata Bima ni Mdogo hivyo ni vyema kuendelea kutoa elimu ili Wananchi wapate uelewa wa kutosha na kuweza kujiunga.

 

Aidha amewaagiza kuangalia njia zitakazoweza kuanzisha Bima ya Makundi ya Watu maalum ikiwemo Wakulima,Wavuvi ,Wafugaji,Wajasiriamali na Wafanyabiashara wadogo wadogo ili iweze kuwasaidia na pia kuiingizaia Serikali mapato kupitia sekta ya Bima.

 

Akitoa maelezo katika kikao hicho Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Mussa Juma amesema wameweka mikakati mengi ya kusaidia Wananchi ikiwemo kuhakikisha wanayawekea mfumo wa kupata Bima hata Makundi ya Cini lakini malengo hayo hayatoleza kufikiwa bila mashirikiano na Serikali hivyo ameiomba Serikali kuunga mkono kwa hali na mali.

 

Nao Viongozi wa TIRA na Makampuni ya Bima wamesema ili kuweza kufikia Uchumi wa Buluu Sekta ya Bima inamchango mkubwa hasa katika ulinzi hivyo wamejiandaa kuanzisha Bima ya Uvuvi ili iweze kuwasaidia.

 

Hivyo ameiomba Serikali kushirikiana ili malengo yaweze kufikiwa ambapo kwa upande wa Tanzania bara wameshaanzisha Bima ya Kilimo.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.