Habari za Punde

Waziri Wa Elimu Na Mafunzo Ya Amali mgeni rasmi katika Mahafali ya sita ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume Mbweni Zanzibar

Waziri Wa Elimu Na Mafunzo Ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akimtunuku cheti mmoja wa wahitimu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt Idrissa Muslim Hija nae akitoa nasaha zake alipopata fursa ya kumkaribisha Waziri Wa Elimu Na Mafunzo Ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akitoa katika Mahafali ya sita ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume Mbweni Zanzibar
Waziri Wa Elimu Na Mafunzo Ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akitoa Hotuba katika Mahafali ya sita ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume Mbweni Zanzibar
Baadhi ya wahitimu akisubiri kupewa vyeti vyao  katika Mahafali ya sita ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume Mbweni Zanzibar
Na Maulid Yussuf , WEMA

 Waziri Wa Elimu Na Mafunzo Ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said amewatunuku vyeti wahitimu wa Stashahada na Shahada ya kwanza wa Tasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume katika fani mbali mbali.

Akizungumza katika Mahafali ya sita ya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume Mhe Simai amewataka wahitimu hao kuitumia Elimu waliyoipata Chuoni hapo kwa manufaa yao, familia zao na Taifa kwa ujumla.
Aidha Mhe Simai ametoa wito kwa Wizara inayohusika na Nishati kuweza kushirikiana na Wizara ya Elimu ili kuiendeleza idara ya Nishati kupitia Taasisi ya Karume kwa kuhakikisha wanapatikana wataalalu bora kutoka katika Chuo hicho.
Mhe Simai amesema miongoni mwa maagizo 13 ya Mhe Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi la kuwataka Mawaziri kuzifanyia marekebisho sheria ambazo zenye vikwazo, Mhe Simai ameutaka uongozi wa Taasisi ya Karume kuhakikisha wanazipitia sheria zao ikiwa zinahitaji kufanyiwa marekebisho zifanyiwe kwa haraka ili kuleta maendeleo zaidi katika elimu.
Pia ameutaka uongozi wa Taasisi ya Karume kushirikiana na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA kila wanapohitaji kwani lengo ni kukuza vipaji vya Wanafunzi wao na kuhakikisha nchi inapata wataalumu wake.
Pia Mhe Simai ameeleza kuwa kuna baadhi ya Wanafunzi bado hawajiamini katika utendaji wa kazi zao wanapopata nafasi za kazi, ambapo amewataka Wakufunzi kuwajenga Wanafunzi wao kuweza kujiamini popote pale watakapo kwenda.
Nae Mkuu wa Taaluma wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume ambae pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt Idrissa Muslim Hija ameuomba uongozi wa Taasisi hiyo kuzichangamkia kwa haraka fursa mbali mbali ambazo zinatokea kwani zitaifanya Taasisi hiyo kutambulika zaidi ndani na nje ya nchi.
Pia ameeleza furaha yake juu ya kufanikiwa kwa Taasisi hiyo kuweza kuanzisha shahada ya urubani na kuitaka kuzidisha mashirikiano na Vyuo vyengine ili waweze kupata ujuzi zaidi.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Taasisi ya karume Bw. Mustafa Ali Garu amewataka wahitimu kuwa makini katika kazi zao wanapopata nafasi za kazi au kujiajiri wenyewe ili kuepuka kukipatia sifa mbaya Chuo chao.
Pia amesema miongoni mwa changamoto ziazowakabili hivi sasa ni uhaba wa madarasa pamoja na dakhalia kutokana na ongezeko la Wanafunzi kwa kila mwaka, hivyo ameuomba uongozi wa Wizara ya Elimu kuliangalia kwa kina suala hilo.
Nae Mwenye kiti wa Baraza la Karume Bi Afua Khalfan Mohd amesema kuwa Tasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume inampango wa kujitangaza ndani ya nchi na nje ya nchi lakini pia kuweza Kuuza Wanafunzi wanaotoka katika Tasisi yao ili waweze kuthaminiwa ndani na nje ya nchi
Hata hivyo ameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuongezewa bajeti ili waweze kuikuza Taasisi hiyo zaidi.
Mapema Rais Mstaafu wa Serikali ya Wanafunzi katika Taasisi ya karume Ndugu Ibrahim Mustafa Ali akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake ameeleza kuwa kwa upande wa Shahada ya kwanza Tassisi imepiga hatua kubwa kwa kuanzisha Shahada nyengine mbili kwa mwaka mpya wa masomo 2020/2021katika fani mbalimbali.
Pia ameeleza Tasisi yao kila mwaka imekuwa ikizalisha watalamu wazuri wenye kuleta ufanisi wa taaluma za kiufundi.
Jumla ya Wanafunzi 447 wametunikiwa Shahada na Stashahada ikiwa 13 kati ya hao wametunikiwa Shahada ya kwanza fani ya urubani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.