Habari za Punde

Wazazi watakiwa kushirikiana na Walimu wa Madrasa

Mwanakikundi cha Vikoba Wilaya ya Kusini Salama Ali Hamadi akisoma Risala ya kikundi hicho katika Uzinduzi wa Kikundi huko Ofisi ya Chama Wilaya ya Kusini .

Mwakilishi Viti Maalum Kundi la Watu wenye Ulemavu Mwantatu Mbarak Khamis akimkabidhi shilingi Milioni Moja Mwenyekiti wa Kikundi cha Vikoba Wilaya ya Kusini Aziza Mnyimbi Makame katika hafla ya Uzinduzi wa Kikundi hicho huko Ofisi ya Chama  Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Mbunge wa Viti Maalum Nafasi za Wanawake Mwatum Dau Haji akikabidhi shilingi Milioni Mbili kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kusini Abdul-azizi Hamadi Ibrahim huko Ofisi za Chama Mkoa wa Kusini Unguja .

Mwalimu Msaidizi wa Madrasatul-sanaa Muntaha Al-Kalamu akikabidhiwa Komputa kwa ajili ya  matumizi ya Chuo hicho na Mbunge wa Viti Maalum Nafasi za Wanawake Mwatum Dau Haji huko Ukongoroni Wilaya ya Kati.

Picha na Maryam Kidiko/Maelezo Zanzibar.

Bahati Habibu Maelezo Zanzibar. 3/1/2021

Wazazi na Walezi wametakiwa kushirikiana na walimu wa madrasa katika  kuwalea Watoto katika misingi  ya dini ya kiislam  ili  kupata vijana wenye malezi bora, upendo uzalendo na kujenga taifa bora na kuepusha vitendo vya udhalilishaji nchini.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vitendea kazi kwa madrasatul Sanaa muntahal-kalam Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kusini Unguja bi Mwatumu Dau Haji huko Ukongoroni amesema dini inamchango mkubwa katika kuwajenga watoto kiimani na hatimae kupata kizazi chenye nidhamu nchini.

Amesema elimu ya dini hasa Qur-an inamaelekezo mazuri na haikuacha kitu katika suala la malezi na namna jamii inavyotakiwa kuishi hivyo amewataka wanajamii kuifuata ili kupunguza vitendo vya udhalilishaji hasa kwa watoto ambao wamekuwa wahanga wakubwa wa kadhia hiyo.

‘’Ikiwa tunataka vitendo vya udhalilishaji viondoke basi tufuate misingi na miongozo iliyomo katika kitabu cha Qur-an na mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W) hivyo ni vyema wazazi walimu na walezi kuzitumia madrasa katika kutoa malezi bora” alisema Mbunge huyo.

Katika hafla hiyo Mbunge huyo alikabidhi mabusati na Kompyuta moja yenye thamani ya shilinngi laki tano thamanini kwa madrassa hiyo ili kuendeleza madraza hiyo.

Sambamba na hayo mbunge huyo alipata fursa ya kukutana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya Kusini Unguja ambapo alichangia jumla ya shilingi milioni mbili kwa ajili ya shughuli za kichama za wilaya hiyo.

Aidha amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja kutumia fedha zinazotolewa na viongozi wa chama hicho kwa maslahi ya chama na Jumuiya zake.

Wakati huo huo Mbunge huyo alizindua Kikiundi cha Vikoba Wilaya ya  kusini Unguja na kuchangia Jumla ya shilingi Milioni Mbili kwa ajili ya kukiendesha kikundi hicho ili kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wao Wawakilishi wa Viti maalum Wanawake Mkoa wa Kusini Unguja walichangia Jumla ya shilingi Milioni mbili na nusu katika Kikundi cha Vikoba Wilaya ya Kusini Unguja.

Akizungumza kwa niaba ya wanakikundi hicho Bi Salama Ali Hamadi amesema lengo kuu la Kikundi hicho ni kuweka na kukopa pesa ili kupunguza umasikini kwa kufanya biashara na kusomesha Watoto.

Kikundi cha Vikoba Wilaya ya Kusini kimeanzishwa 2014 kikia na Wanachama 30 Wanawake.  

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.