Habari za Punde

Wilaya ya Kusini yaongoza kwa ajali za barabarani

 Na Mwashungi Tahir   Maelezo       

Imeelezwa kwamba Wilaya ya Kusini Unguja zimeripotiwa kuwa na ajali nyingi ajali (6) ukilinganisha na Wilaya nyengine  ikifuatiwa na Wilaya  ya Kaskazini ‘B’ ajali (5).

Hayo ameyasema Mtakwimu kutoka kitengo cha Takwimu za ajali na makosa barabarani Afisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Asha Mussa Mahfoudh huko katika ukumbi wa Mtakwimu Mkuu uliopo Mazizini wakati akizungumza na waandishi wa habari   akiwasilisha takwimu za ajali  na makosa barabarani.

Amesema  kwamba jumla ya ajali 26 za ajali za barabarani zimeripotiwa mwezi wa Desemba 2020.

Amesema  mlinganisho wa idadi ya   ajali kwa mwaka uliopita imeongezeka kwa asilimia 4.0 kutoka ajali 25 kwa mwezi wa Disemba, 2019 hadi ajali 26 mwezi wa Disemba 2020.

Pia amesema kwa upande wa ajali kwa mwezi uliopita imeongezeka kwa asilimia 23.8 kutoka ajali 21 kwa mwezi wa Novemba , 2020 hadi 26mwezi wa Desemba, 2020.

Mtakwimu huyo akiwataja waathirika wa ajali za barabarani ni pamoja na madereva, abiria, wapanda baiskeli na pikipiki  na wanaotembea kwa miguu.

Na miongoni mwa makosa makuu yanayoongoza kwa Wilaya ya Mjini, Magharib A na B  ni pamoja na kushindwa kuvaa bejikwa utingo na dereva wa gari za abiria,kutofuata miongozo ya kanuni za usalama barabarani , kuendesha chombo cha moto vespa, gari,pikipiki na fifti bila ya leseni ya njia, kuendesha chombo cha moto bila ya helmet na kuzidisha idadi ya abiria na mizigo.

Vile vile amesema kwa upande wa makosa ya Barabarani jumla 1,320 yameripotiwa mwezi wa Desemba, 2020 ambapo makosa 1,317 yamefanywa na wanaume na matatu  yamefanywa na wanawake.

Kwa upande wa Wilaya ya Kati ina idadi kubwa ya makosa ya barabarani  ambapo makosa 247 sawa na asilimia 18,7 kati ya makosa yote yaliyoripotiwa .

Na upande wa Micheweni alisema ina idadi ndogo ya makosa ya barabarani yaliyoripotiwa ni 30 sawa na asilimia 2.3.

Akitoa takwimu za ajali barabarani  kwa mwaka 2020 jumla ua ajali zimeripotiwa kwa mwaka 2020 na miongoni ya walioathirika wanawake 83 asilimia 15.0 , waliofariki 18 waliojeruhiwa 68, na wanaume 469swa na asilimia 85.0waliofariki 162 na waliojeruhiwa 307.

Nae Koplo Ali Abdullah Juma kutoka Ofisi ya Mkuu wa Usalama wa barabara Polisi Zanzibar amesema katika mwaka 2021 wamejipanga kupunguza ajali barabarani kwa kuondosha magari yote yaliyokuwa mabovu.

Na pia madereva wataosababisha ajali kwa uzembe watazuiliwa leseni zao na kurudishwa tena kwenye vyuo kujifunza zaidi.

Kwa upande wake Khamis Mwinyi Bakari Mkaguzi msaidizi wa Polisi,Mkuu wa Kitengo cha Takwimu za uhalifu kutoka Makao Makuu ya Polisi Zanzibar amewataka madereva kuwa makini kuepukakusababisha  ajali kwa waendao kwa miguu, wapanda baiskeli kwani kutaweza kuwasababishia ajali au vifo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.