Habari za Punde

Mahafali ya 20 ya Chuo cha Kikuu cha Abdulrahman Al Sumait Chukwani leo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na (kulia kwake) Rais Mstaaf wa Zanzibare Awamu ya Sita Mhe.Dkt. Amani Karume na (kushoto kwake) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said, wakiwa katika maandamano ya Wanachuo wakielekea katika viwanja vya Chuo hicho kwa ajili ya Mahafali ya 20 yaliofanyika leo 27-2-2021.Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Abdulraham Al Sumait Chukwani Zanzibaer wakiwa katika viwanja vya Chuo wakihudhuria hafla ya Mahafali ya 20 ya Chuo hicho yaliofanyika leo katika viwanja vya Chuo Chukwani Zanzibar.

Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said wa kwanza kushoto, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe Leila Mohammed Mussa wa pili kushoto pamoja na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Balozi Mubarak Mohammed Alshaigan, katikati, pamoja na uogozi wa Chuo kikuu cha Abdulrahman Alsumait, wakikagua library ya chuo hicho baada ya kumaliza mahafali ya 20 ya wanafunzi katika viwanja vya Chuo hicho Chukwani Mjini Unguja.

Na Maulid Yussuf WEMA

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.