Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Ustawi wa Jamii Duniani

 Washirki wakisikiliza  kwa umakini  hotuba ya Mgeni Rasmi Iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi ''A'' Suzan Peter Kunambi kwa niaba Waziri  wa  Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ. Masoud Ali Mohammed katika kuadhimisha Siku ya Ustawi wa Jamii Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Jumanne ya Tatu ya mwezi wa Tatu ya kila Mwaka. maadhimisho hayo yamefanyika huko Ukumbi wa Idriss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.

 Jamila Borafiya Hamza (Wapili kulia )  na Awena Hassan Seif ( Wenye Ulemavu wa Uwoni) wakisoma utenzi katika Maadhimisho ya  Siku ya Ustawi wa Jamii Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Jumanne ya Tatu ya mwezi wa Tatu ya kila Mwaka. maahimisho yaliofanyika  Ukumbi wa Idriss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Usatawi wa Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Bi Abeda Rashid Abdallah akizungumza katika Madhimisho ya  Siku ya Ustawi wa Jamii Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Jumanne ya Tatu ya mwezi wa Tatu ya kila Mwaka. maahimisho yaliofanyika katika Ukumbi wa Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.

, Mkuu wa Wilaya ya Magharibi ''A'' Suzan Peter Kunambi akisisitiza jambo wakati akisoma hotuba  kwa niaba Mgeni Rasmi    Waziri  wa  Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ. Masoud Ali Mohammed katika kuadhimisha Siku ya Ustawi wa Jamii Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Jumanne ya Tatu ya mwezi wa Tatu ya kila Mwaka. maahimisho yaliofanyika katika  Ukumbi wa Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.

 Mkuu wa Wilaya ya Magharibi ''A'' Suzan Peter Kunambi akisoma hotuba  kwa niaba ya Mgeni Rasmi    Waziri  wa  Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ. Masoud Ali Mohammed katika kuadhimisha Siku ya Ustawi wa Jamii Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Jumanne ya Tatu ya mwezi wa Tatu ya kila Mwaka. maahimisho hayo yamefanyika huko Ukumbi wa Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.


PICHA NA BAHATI HABIBU/HABARI MAELEZO.

Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar                      16/3/2021

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Zanzibar, Mh. Masoud Ali Mohamed amewataka Maafisa wa Vijana, Wazee na Watoto kushirikiana na Maafisa wa Ustawi wa Jamii kwa lengo la  kupambana na tatizo la udhalilishaji nchini.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi ‘A’. Suzan Peter Kunambi  kwa Niaba ya Waziri huyo katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakili Kikwajuni wakati wa kuadhimisha Siku ya Ustawi wa Jamii Duniani.

Amesema Serikali na Taasisi za Ustawi wa Jami pamoja na Wadau mbalimbali wanatambua juhudi kubwa na mchango wa wana Ustawi wa Jamii Duniani ambao unazoshughulikia masuala ya jamii hivyo hakuna budi kuunga mkono juhudi hizo ili kuhakikisha haki za binadamu na maendeleo ya jamii zinapatikana.

Amesema Wana Ustawi wa Jamii wanatoa huduma mbalimbali kwa jamii na kuchambua mahitaji na changamoto za wateja wao kwani wao ni watetezi wa jamii kwa kupata mahitaji yao kwa lengo ya kuboreha  mustakabali wa maisha.

“Ninafahamu pia Maafisa Ustawi mna changamoto nyingi zinazowakabili ikiwemo vitendea kazi vinavyosaidia  kurahisisha utendaji kazi katika kukabiliana na matatizo na kufikia walengwa (clients).nawataka wanajamii kwa ujumla kufanya kazi kwa moyo wa uzalendo kwa kuzingatia fursa zilizomo katika nchi yetu.”Alisema Waziri Masoud 

Pia amesema kuwa kuadhimisha siku hiyo kunatathmini juhudi na michango inayotolewa na Maafisa  Ustawi wa Jamii, Wadau wa Ustawi Jamii  na Wasaidizi wa Maafisa Ustawi kwa maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Aidha Waziri huyo amefahamisha kuwa Wana Ustawi wa Jamii wanajukumu la kudhibiti majanga katika jamii zao, kwani wanafanya kazi katika maeneo tofauti yakiwemo Hospitalini, Vituo vya kutetea haki za Wazee na Watoto, Mahakamani, Vyuo Vikuu, Polisi, Magereza, Skuli, pamoja na Asasi za kiraia.

Aidha amesema kuwa Kwa mwaka huu Idara ya Wazee na Ustawi wa Jamii pamoja na Taasisi ya ustawi wa jamii Zanzibar (ZASWA) wanaadhimisha siku hiyo kwa kujumuika na Taasisi mbalimbali ikiwa ni moja shirikisho la Jumuiya za Kimataifa za Wanaustawi wa Jamii  Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, kuhamasisha mshikamano wa kimataifa ili kutambua michango ya wanaustawi wa jamii Duniani kote.  

Nao wawakilishi kutoka Taasisi zinazosaidia Vijana katika masuala ya Ustawi wa Jamii wamesema kuwa wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa rasilimali  fedha na vitendea kazi na kupelekea kutofikia malengo waliojiwekea

Hata hivyo Taasisi hizo zimeiomba Serikali kuwapatia mikopo kwa vijana wanaotaka kusomea fani ya Ustawi wa Jamii pamoja na vitendea kazi ambavyo vitafanikisha malengo waliojiwekea.

Maadhimisho hayo ni ya kwanza kufanyika Zanzibar ambayo yalifanyika leo tarehe 16 March. Maafisa wa Ustawi wa Jamii walifanya vipindi vya kutoa Elimu ya Ustawi wa Jamii kupitia Televition na redio, ambapo KAULI MBIU YA MWAKA HUU NI MIMI NILIVYO NI KUTOKANA NA SISI TULIVYO.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.