Habari za Punde

Matukio ya Picha Kisiwani Pemba.

BAADHI ya wafanyakazi wa Shirika la Umeme Zanzibar ZECO Tawi la Pemba na wananchi wa shehia ya Mgelema Wilaya ya Chake Chake, wakikata mti wa mzambarau ambao matawi yake yameangukia katika laini kubwa ya Umeme, mti ambao ulidaiwa kutiwa moto na watu wasiofahamika na kusababisha wananchi kukosa huduma hiyo
WAFANYAKAZI wa Shirika la Umeme Zanzibar Tawi la Pemba, wakishirikiana na wananchi wa shehia ya mgelema Wilaya ya Chake Chake, wakiwa katika harakati za kuwachia waya wa laini kubwa ya umeme, baada ya mti ulioangukiwa waya huo kuondolewa ili waweze kurudisha huduma ya umeme katika shehia hiyo

WAANDISHI wa habari wa shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar Ofisi ya Pemba, Habiba Zarali na Suhura Juma wakifahamisha kwa vitendo juu ya uwekaji wa habari zinazohusiana na wanawake na uongozi katika mitandao ya kijamii, baada ya kupatiwa mafunzi ya matumizi ya mitando na TAMWA Pemba.

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.