Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega akiongea na wachezaji na wananchi waliofika Uwanja wa Ushirika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro kwenye Mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika leo Februari 28, 2021. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Rajabu Kundya na shoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Irene Mtiganzi.
Na
Eleuteri Mangi, WHUSM-Moshi
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega amewataka
waandaaji wa Mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon wawe wabunifu na kuongeza
vionjo vipya kwenye mashindano hayo ili kuwavutia watu wengi zaidi kuja
kushiriki mashindano na kuja kujionea vivutio vizuri vilivyopo katika mkoa wa
Kilimanjaro na taifa kwa kwa ujumla.
Naibu
Waziri Ulega amesema hayo leo Februari 28, 2021 alipokuwa akifunga Mashindano
ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika Uwanja wa Ushirika Manispaa
ya Moshi.
“Ninyi
kama wataalamau wenye uzoefu angalieni na muongeze ubunifu ili kuboresha
mashindano haya, wanapokuja watu hapa uchumi uendelee kukua zaidi ambapo
wajasiriamali waendee kupata pesa zaidi na wenye kuuza baishara ndgondogo
waendendelee kupata pesa zaidi tujenge uchumi wetu” amesema Naibu Waziri Ulega.
Pia
amewataka waandaaji wa mashindano hayo hayarudi nyuma yanasonga mbele na yawe
na ubunifu na yaweze kutangazika zaidi duniani kote ili kuwavuta wakimbiaji
wengi wenye majina makubwa duniani waje kushiriki mashinfdano hayo.
Aidha,
Naibu Waziri Ulega amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli amewaonesha Watazania namna nzuri ya kuiwekezaji na fursa
za kibiashara katika taifa letu bado zipo wazi ambapo maboresho hayo
yakifanyika yatawavuta wawekezaji wengi zaidi waje kuwekeza nchini.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Moshi Rajabu Kundya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo
Anna Mughwira ameishukuru Serikali kupitia Wizara yenye dhamana ya michezo
nchini ambapo amesema mashindano hayo yamekuwa chachu ya kuwakutanisha wananchi
kutoka mikoa mingine na mataifa mbalimbali kwa kuwa zimeshiriki zaidi ya nchi
55.
Wataalamu
wa afya wametuhakikishia akili safi daima hukaa kwenye mwili safi, na mwili
safi ni ule ambao haujachokonolewa na maradhi na namna pekee ya kuulinda mwili
ni kufanya mazoezi na kulinda afya ya mwili na akili, hii ilikuwa ni fursa
muhimu ambapo amewasihi Watanzania tuendelee kufanya mazoezi kujiandaa na
mashindano yajayo.
Naye
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Irene Mtiganzi ambao ni moja ya wa dhamini ya
mashindano amesema kampuni yao inajivunia kuwa na mchango katika kukuza utalii
wa michezo nchini hatua inayosaidia kuongeza watalii wa ndani nan je ya nchi
katika viutio mbalimbali vilivyopo katika mkuo huo.
Mshindi
wa kwanza katika mbio za km 42 kwa wanaume na wanawake amepata zawadi ya
Shilingi milioni 4,100,000 kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo na
kuongezewa kiasi cha Shilingi 1,500,00 ikiwa motisha kwa Watanzania waliofanya
vizuri kwenye mashindano hayo na kufanya jumla ya fedha walizopokea jkufikia
kiasi cha Shilingi 5,600,000.
Mashindano
ya Kilimanjaro marathon ya mwaka huu ni ya 19 kufanyika tangu kuanzishwa kwake 2003
ambayo yameshirikisha wachezaji zaidi ya elfu 12 kutoka nchi zaidi ya 55 ambapo
Watanzania wamefanya vizuri katika mbio za km 42 kuanzia mshindi wa kwanza
ambaye ni Augustino Sule aliyekimbia kwa 2:18:04 kwa upande wa wanaume huku kwa
upande wa wananwake Watanzania wameongoza kuanzia mshindi wa kwanza ambaye ni
Jackline Sakilu aliyekimbia kwa 02:45:44 hadi nafasi ya tisa wakati nafasi ya
10 imechukuliwa na Dominic Kremer raia kutoka nchini Netherland.
No comments:
Post a Comment