Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi akutana na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi Ikulu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifuatilia Muktasari wa Taarifa ya Utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwa Mawaziri na Makatibu Wakuu wakati alipowaapisha, ikiwasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais ) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.(Picha na Ikulu)
WAKUU wa Idara za Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi wakifuatilia mkutano huo wa kuwasilisha ripoti ya utekelezaji wa maagizo ya Rais aliyoyatowa kwa Mawaziri na Makatibu Wakuu wakati alipowaapisha, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Ndg.Thabit Idarous Faina, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Rais aliyoyatoa kwa Mawaziri na Makatibu Wakuu wakati wa kuwaapisha, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. na (kulia kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 3-3-2021 na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na (kulia kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.(Picha na Ikulu)
WAKUU wa Idara za Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi wakifuatilia mkutano huo wa kuwasilisha ripoti ya utekelezaji wa maagizo ya Rais aliyoyatowa kwa Mawaziri na Makatibu Wakuu wakati alipowaapisha, mkutamo huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza wakati wa mkutano huo wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Rais wakati wa kuapishwa kwa Mawaziri na Makatibu Wakuu, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.