Habari za Punde

Wanahabri Zanzibar Wabuni Tunzo Kwa Dkt.Mwinyi na Maalim Seif.

 

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya waandishi wa habari Dkt,Mzuri Issa akizungumza na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi kuhusu maadhimisho ya siku ya waandishi wa habari na mikakati waliojipanga.

Kamati ya maadalizi ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya masomo ya habari ya chuo kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA)Kilimani mjini Unguja.

Na Muhammed Khamis.TAMWA-Zanzibar 

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Dkt,Mzuri Issa Ally amesema wameamua kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari kivyengine kuliko  miaka yote iliowahi kupita nyuma.

Mwenyekiti huyo ambae ni Mkurugenzi wa TAMWA-Z’bar aliyasema hayo wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari katika viunga  vya  kitivo cha idara ya ya mawasiliano ya chuo kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kilimani mjini Unguja.

Alisema kwa mwaka huu  kamati hio wameamua kuja na muonekano mpya na utakua wakipekee kuliko miaka yote iliopita nyuma kutokana na kuipa umuhimu siku hio adhimu kwa waandishi wa habari ambayo kila mwaka hufanyika mara moja pekee.

Akieleza baadhi ya mikakati waliojiwekea ni pamoja na kuanzishwa kwa tunzo za waandishi wa habari  katika makundi matano tofauti.

Wakati akifafanua makundi ya tunzo hizo alisema ni pamoja na tunzo ya uchumi wa buluu ambayo wameamua kuipa jina la Dkt,Mwinyi ‘’Award’’ kundi la pili kiliwa ni tunzo ya uandishi wa  habari za Serikali  ya umoja wa kitaifa ambayo nayo imepewa jina la Maalim Seif ‘’Award’’.

Aidha Mkurugenzi huyo amendelea kutaja makundi mengine ambayo ni uandishi wa habari za jinsia ambayo imepewa jina la Mariam Mwinyo ‘’Award’’ na nyengie tunzo ya maswala ya kodi ambayo imepewa jina la ZRB ‘’Award’’huku tunzo nyengine ikilenga maswala ya rushwa na uwajibikaji ambayo imepewa jina la ZAECA ‘’Award’’

Akifanunua zaidi alisema mashindano hayo kwa waandishi wa habari yatazingatia  kazi zote zilizotolewa kwenye vyombo vya habari kuanzia mwezi januari mwaka huu hadi mwishoni mwa mwezi wanne mwaka huu.

Alisema uwepo wa tunzo hizo ni muhimu mno pia itasaidia na kuongeza  uwajibikaji         Serikalini kwa kuwa tunzo hizo zimezingatia mambo muhimu yanayomgusa kila mtu. 

‘’Mashindano haya hayatamalizia hapa na tunaamini pia yatakuza vipaji vya waandishi wetu wacha hapa Zanzibar na itawafanya waweze kujituma zaidi’’aliongezea.

Awali Mwenyekiti wa kamati hio mwandishi wa habari mwandamizi wa ITV Farouk Kareem aliwataka waandishi wa habari kujitokeza kwa wingi kuwania tunzo hizo ambazo ni mara ya kwanza kutolewa visiwani hapa.

Alisema licha ya uwepo wa tunzo hizo lakini pia kutakua na bonanza maalumu la michezo kwa waadishi wa ahari litakalolenga kuhamaisha ufanyaji wa mazoezi kwa wanahabari visiwani hapa.

Maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari ulimwenguni hufanyika kila ifikapo tarehe 3 ya mwezi wa tano ya kila mwaka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.