Habari za Punde

Wilaya ya Korogwe na Kero ya Huduma za Jamii.

Na Hamida Kamchalla, KOROGWE.

WANANCHI wilayani Korogwe wametolewa kero zao za ukosefu wa huduma muhimu za kijamii zikowemo maji, umeme, miundombinu ya barabara na elimu ambazo baadhi ya maeneo ya vijijini kukosa kabisa huduma ya umeme.

Akiongea kwa niaba ya wananchi wa jimbo la Korogwe vijijini, mbunge Timotheo Mzanva alisema kero ni nyingi na sinazidiana kwa ukubwa lakini ukiachia ya maji na kukatika kwa umeme kuna vijiji takribani 40 havina maji kwa upande wa jimbo lake na kuiomba serikali kuwapa kipaumbele katika kuwaletea wananchi wake huduma hiyo.

"Muheshimiwa Makamu wa Rais, pamoja na serikali kufanya mengi mazuri lakini pia tuna kero, mkuu wa wilaya kaongelea za hapa mjini, lakini wakati anaongelea kukatika kwa umeme, madiwani wangu wakaangaliana wakijishangaa wenzetu wanalalamika kukatika kwa umeme wakati kwetu vijiji 47 haviba umeme kabisa" alisema.

Mzanva alibainisha kero ya miundombinu ya barabara na kukatika kwa madaraja ambapo suala la bajeti limekuwa kitendawili kwakuwa haitoshelezi katika kuboresha miundombinu hiyo ambayo kuna daraja la Mswaha lilivunjika tangu mwaka 2003 hadi sasa halina matengenezo.

"Serikali inetuahidi kutupatia umeme katika vijiji hivi kwa awamu lakini kuna kero nyingine sugu zaidi ya miundombinu, barabara zetu vijijini ni mbovu sana na kuna madaraja yaliyovunjika na hayana matengenezo, tunaomba kama bajeti haitoshi itengwe hata pesa ya majanga ili tutengenezewe miundombinu yetu" aliongeza.

Hata hivyo aliiomba serikali kuangalia jinsi ya kufanya mpango mkakati wa kupeleka ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) baada ya eneo lililotengwa kujengwa chuo hicho wilayani humo kuhamishiwa mjini wakati wananchi walijitolea nguvu zao kusafisha, hivyo ili kutowakatisha tamaa katika kushiriki shuhuli za maendeleo inapaswa kuwapelekea ujenzi huo.

Naye mbunge wa Korogwe mjini Winfred Kimea alisema pongezi nyingi kwa serikali kwa utekelezaji wa hali ya juu lakini alisema picha ya mji huo awali haikukaa sawa kutokana na kukosa viwanda, lakini kwa juhudi za serikali kufanya ushawishi kwa wawekezaji imechangia kupata kiwanda cha kusindika matunda na kusisitiza suala la ajira lipewe kipaumbele kwa wazawa.

"Mji wetu hapo nyuma haukuwa ukileta taswira yake kwa kukosa kiwanda hata kimoja, tunashukuru serikali kufanya juhudi za kumtafuta muwekezaji na kumshawishi kuleta kiwanda, lakini kilio changu kingine kiwanda kile kitoe kipaumbele kwa vijana wazawa ili wapate ajira na kunufaika na mji wao" alisema.

Hata hivyo Kimea alisema kwa upande wa elimu bado kuna tatizo la uhaba wa shule ambalo hasababisha wanafunzi kusongamana wawapo shuleni na madarasani jambo ambalo wengine hukosa ari ya kusoma na kuishia kutoroka na kuchangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu.

"Tunashukuru kwa kupata matumaini ya kuongezewa shule wilayani kwetu, tumeongea na Waziri Ndalichako amesema serikali ina mpango wa kuongeza shule elfu moja nchini na kati ya hizo wilaya yetu imebahatika, tunamuomba Waziri atupe kipaumbele kutuongezea japo nne ili watoto wetu wapate nafasi pana ya kusoma" aliongeza Kimea.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Kissa Gwakisa alifafanua utaratibu wa kupatiwa ufumbuzi wa umeme na kuongeza kuna kero nyingine kubwa ya maji ambayo pia iko kati ya wilaya 28 ambazo ziko kwenye mpango wa kumaliziwa tatizo hilo huku akitoa shukurani zake kwa Wizara husika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.