Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile
akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu (wanaomsikiliza)
wakati akiwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo
kwa mwaka 2021/22 Bungeni, Dodoma
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani
Kakoso akichangia hoja baada ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
Dkt. Faustine Ndugulile (wa tatu kushoto aliyeketi) kuwasilisha taarifa ya
makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2021/22 ya Wizara hiyo kwa wajumbe wa
Kamati hiyo Bungeni, Dodoma. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo,
Mhandisi Kundo A. Mathew na wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Dkt. Zainab Chaula
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo
Mathew (wa kwanza kulia) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt.
Zainab Chaula mara baada ya Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile kuwasilisha
taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2021/22 kwa
wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Bungeni, Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Anne
Kilango Malecela na mjumbe wa Kamati hiyo, Ally Jumbe wakipitia taarifa ya Waziri
wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo
pichani) kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka
2021/22 baada ya kuwasilisha kwenye Kamati hiyo Bungeni, Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Masache Kasaka
akichangia hoja baada ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt.
Faustine Ndugulile (hayupo pichani) kuwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato
na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2021/22 kwenye kikao kilichofanyika
Bungeni, Dodoma
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakimsikiliza Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) wakati akiwasilisha taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2021/22 kwenye kikao kilichofanyika Bungeni, Dodoma.
Picha na Prisca Ulomi
No comments:
Post a Comment