Habari za Punde

Jumuiya ya Watu Wenye Ulemavu Shauri moyo Yawezeshwa Vifaa vya Kazi.

Mwakilishi wa viti maalum walemavu Mwanatatu Mbaraka Khamis akimpatia maelekezo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walemavu Shaurimoyo (JUWASHA) Juma Abdalla Juma mara baada ya kumkabidhi fedha taslim kwaajili ya wana ushirika wa "HAYAWI HAYAWI HUWA " wanaotakakujishuhulisha na ususi wa ukindu katika ofisi ya JUWASHA Shaurimoyo Zanzibar..
Mwakilishi wa viti maalum walemavu Mwanatatu Mbaraka Khamis akiwakabidhi watendaji wa Jumuiya ya Walemavu Shauri Moyo mashine za mapishi kwaajili ya  wana ushirika wa "HAYAWI HAYAWI HUWA "waliojikita katika fani ya mapishi huku ofisi za JUWASHA Shauri moyo Zanzibar.

Katibu wa  Jumuiya ya Walemavu Shauri Moyo Said Yakub Hassan  akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Juwasha mara baada ya kukabidhiwa mashine za mapishi na  Mwakilishi wa viti maalum walemavu Mwanatatu Mbaraka Khamis ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake alizoziweka huko Ofisi za JUWASHA Shaurimoyo Zanzibar.

PICHA NA FAUZIA MUSSA / MAELEZO ZANZIBAR.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.