Habari za Punde

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA WATENDAJI WA SEKTA YA MAJI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa malori matatu ya kunyonya majitaka ambayo aliyakabidhi kwa Halmashauri za Miji ya Kahama, Tanga na Lindi baada ya Waziri Mkuu kuhutubia Mkutano wa Watendaji wa Sekta ya Maji kwenye ukumbi wa Chuo hicho jijini Dodoma, Mei 11, 2021. Wengine pichani kutoka kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu, Naibu Waziri wa  Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi, Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, William Tate Ole Nasha na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji  Mhandishi Anthony Sanga. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso  (wa pili kulia) wakikagua pikipiki 147 ambazo zimenunuliwa na Wizara ya Maji na zimekabidhiwa  kwa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA). Makabidhiano hayo yamefanyika  kwenye viwanja vya Ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma baada ya Waziri Mkuu kuhutubia Mkutano wa Watendaji wa Sekta ya Maji 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mkutano wa Watendaji wa Sekta ya Maji kwenye ukumbi  wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Watendaji  wa Sekta ya Maji wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma. 
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Watendaji  wa Sekta ya Maji wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma, Mei 11, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.